WAZIRI MCHENGERWA AZINDUA BOTI YA KITALII YA TAWA SEA CRUSIER

 WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Mchengerwa amezindua boti ya utalii iitwayo TAWA SEA CRUISER, Machi 14,2023, katika Hifadhi ya Urithi wa Dunia Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara yaliyopo katika Mkoa wa Lindi.


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mhe. Mchengerwa amewataka wananchi kutumia boti hiyo itakayounganisha shughuli za utalii katika kanda ya kusini pamoja na ukanda wa pwani ili kuendelea kukuza utalii wa ndani.

Boti ya TAWA SEA CRUISER yenye uwezo wa kubeba watalii 50 kwa mara moja, imelenga kuimarisha shughuli za usafirishaji wa watalii wanaotembelea katika Hifadhi ya Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara.

Sambamba na hili Waziri Mchengerwa amepokea Meli ya Kimataifa ya watalii iitwayo, LE JACQUES - CARTIER PONANT iliyobeba watalii 90 kutoka nchi ya Ufaransa na Marekani.

Meli hiyo Le Jacques- Cartier Ponant ni meli ya tatu ya Kimataifa iliyotia nanga katika Hifadhi za Magofu ya Kilwa Kisiwani ndani ya kipindi cha wiki moja.




Post a Comment

Previous Post Next Post