TRA YAZINDUA OFISI YA WALIPAKODI WENYE HADHI MAALUMU

 

Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda, Kamishna Mkuu wa mamlaka wa TRA, Mcha Hassan Mcha kushoto na Kaimu Kamishna wa Kodi za Ndani wa TRA, Michael Muhoja wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa ofisi ya walipakodi binafsi wenye hadhi ya juu. Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo Oktoba 15, 2024.

Na Karama Kenyunko Michuzi Tv 
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imezindua ofisi maalamu itakayohudumia walipakodi binafsi wenye hadhi ya juu na kuwahakikishia huduma bora.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ofisi hiyo iliyopo katika jengo la Golden Jubilee, Posta jijini Dar es Salaam Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda amesema, hatua hiyo ni katika kuendelea kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan haswa katika kuhamasisha ulipaji kodi kwa hiyari. 

“Ninayo furaha kuungana na nyie kuja kuizindua ofisi ya walipakodi binafsi wenye hadhi ya juu iliyoanza kazi Oktoba Mosi, mwaka huu,” alisema.

 Amesema, ofisi hiyo itakuwa ikihudumia makundi manne ambayo ni wamiliki wa makampuni makubwa yanayozalisha zaidi ya Sh. bilioni 20 kwa mwaka, wamiliki wa hisa zenye thamani ya Sh. bilioni 2.5 kwa mwaka,wale wote wenye ubia kwenye makampuni zinazozalisha zaidi ya shilingi bilioni 20, viongozi wa mihimili mitatu ya juu na wa taasisi watakaoteuliwa.

Mwenda amebainisha kuwa ofisi hiyo inawalenga walipakodi hao kwa sababu wanataka kuwapatia huduma bora kwa kutambua mchango wao wanaoutoa na unyeti wa shughuli zao.

Mwenda alisema sababu kubwa ya kuanzishwa kwa ofisi hiyo ni kutokana na mchango mkubwa unaotolewa na makundi hayo kwani kushindwa kuyapa huduma stahiki kutasababisha serikali kupoteza mapato na kufanya uchumi wa nchi kushuka.

Akifafanua kuhusu walipakodi wenye hadhi ya juu, amesema  ni wamiliki wameanzisha kampuni ambazo zinalipa kodi katika mamlaka hiyo, wanalipa kodi kupitia mapato yao binafsi na ameajiri watu wanalipa kodi.

“Kwa kuanza tumeanza na walipakodi 158, lakini walipakodi wamiliki binafsi wapo 111 wote wameshaitwa na viongozi  wa mihimili mitatu ya juu ya serikali na wa taasisi 47 watakuja baadaye". Amesema 

Alisema Mamlaka imeanza na idadi hiyo kwani ndio waliokidhi vigezo vya kuhudumiwa katika ofisi hiyo.

Akifafanua kuhusu walipakodi wenye hadhi ya juu, amesema  ni wamiliki wameanzisha kampuni ambazo zinalipa kodi katika mamlaka hiyo, wanalipa kodi kupitia mapato yao binafsi na ameajiri watu wanalipa kodi.

Aliongeza kuwa : “Tunawapa huduma bora kwani mchango wao mkubwa sana, wameanzisha kampuni, wanalipa kodi na viongozi wana mchango mkubwa wana majukumu mengi, lazima tuwarahishishie.”

Mwenda amesema lazima wawe karibu na walipakodi hao, kuhakikisha kile kinachotakiwa kulipwa kinalipwa.

Amesema mamlaka inahitaji kuweka na kuleta usawa katika usimamizi na ulipaji wa kodi kwani watu hawa walikuwa wanalipa kodi lakini si kwa ushahihi sababu makundi waliyokuwepo hayakuwa sahihi pia hata huduma walizokuwa wakipewa huko hazikuwa rafiki kwani kuna watu walikuwa kundi la walipa kodi wakubwa, wakati na walipa kodi wadogo sasa tunawaleta pamoja ilikuweza kutafasiri sheria za kodi.

Aidha ameahidi huduma zitakuwa bora zinazoendana na hadhi yao na kuwaondolea usumbufu kwa kuwasogezea huduma karibu.

Naye, Naibu Kamishna Mkuu wa mamlaka hiyo, Mcha Hassan Mcha amesema ofisi hiyo ni miongoni mwa fursa ya kusogeza huduma karibu na walipakodi, kwa lengo la kuongeza ufanisi wa utendaji kazi ilikusaidia kuwatambua walipa kodi wote na na kufahamu zaidi namna ya ulipaji,ili kuongeza uweledi wa ukusanyaji mapato na kuongeza walipa kodi kwa hiari na kuwahudumia bila changamoto.
Picha ya Pamoja.



Matukio mbalimbali.

Post a Comment

Previous Post Next Post