Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza katika kikao chake na taasisi za umma zinazohusika na huduma za maji ambacho kimefanyika leo jijini Dar es salaam sambamba na kukabidhi mitambo na vifaa vya kisasa vya uchimbaji visima na mabwawa ambavyo vimenunuliwa hivi karibuni na Serikali
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James akizungumzia kuhusu miradi mbalimbali ya maji inayotekelezwa katika wilaya yake.
Mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akizungumza katika kikao cha taasisi za umma zinazohusika na huduma za maji jijini Dar es salaam na kueleza malengo ya Dawasa.
Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Clement Kivegaro akizungumza katika kikao cha taasisi za umma zinazohusika na huduma za maji jijini Dar es salaam na kueleza malengo ya Dawasa.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akikabidhi gari lenye mitambo na vifaa vya kisasa vya uchimbaji visima na mabwawa ambavyo vimenunuliwa hivi karibuni na Serikali.
Baadhi ya washiri kutoka katika taasisi za umma waliojitokeza katika kikao hicho.(picha na Mussa Khalid)
……………………..
NA MUSSA KHALID
Waziri wa Maji Jumaa Aweso amewataka Wakala wa Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa DDCA kuhakikisha wanafufua visima 197 ambavyo vilichimbwa lakini havikufanikiwa kutoa maji ili kuwaondolea wananchi adha ya changamoto ya maji katika kipindi hiki.
Pia amewataka Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira DAWASA kuhakikisha wanafuata ratiba ya mgao wa maji ili kuwapunguzia usumbufu wananchi katika kipindi hiki cha uhaba wa maji
Waziri Aweso ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza katika kikao chake na taasisi za umma zinazohusika na huduma za maji sambamba na kukabidhi mitambo na vifaa vya kisasa vya uchimbaji visima na mabwawa ambavyo vimenunuliwa hivi karibuni na Serikali.
Aidha Waziri Aweso ametumia fursa hiyo kuwataka DAWASA na kuwasisitiza wahakikishe wanafuata ratiba ya mgao wa maji ili kuwapunguzia usumbufu wananchi katika kipindi hiki cha uhaba wa maji
‘Hakuna kipindi ambacho tunatakiwa kuwa wamoja kama kipindi hiki kwani sisi tunajukumu muhimu la kuhakikisha wanaDar es salaam na watanzania wanapata maji kwa wakati kwani tunatambua kuwa DAWASA
Tunauwezo wa kuzalisha maji lita Mill 520 mitambo yetu lakini kwa sasa mitambo yetu inawezo wa kuzalisha lita Mill 300 kwa hiyo tunaupungufu”amesema Waziri Aweso.
Awali akizungumza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James amempongeza Waziri kwa kusimamia na kufanya jitihada za kuhakikisha wananchi wa jiji la Dar es salaam wanapata maji ya kutoka katika kipindi hiki kigumu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange moja ya changamoto wanayokumbana nayo ni vyanzo vya maji na kusisitiza kuwa mradi wa maji wa Kigamboni utasaidia kupunguza changamoto iliyopo.
Hata hivyo Waziri wa Maji Jumaa Aweso amewataka watumishi wa taasisi hizo zilizo chini ya wizara ya maji kushikamana katika kipindi hiki kigumu na kuhimiza utunzaji wa maji.