Madaktari bingwa wa moyo waendelea kutoa huduma za matibabu ya moyo Mkoani Geita

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography - ECHO) mwananchi aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano inayoendelea katika Hospitali hiyo.Mtafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Macklina Komba akimfanyia usajili mwananchi wa Mkoa wa Geita aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano inayoendelea katika Hospitali hiyo.Afisa Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) John Daniel akimpima Shinikizo la damu mkazi wa Chato aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano inayoendelea katika Hospitali hiyo.

Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Kulwa Richard
akimpima wingi wa sukari mwilini mkazi wa Chato aliyefika katika Hospitali ya
Rufaa ya Kanda Chato kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo
wakati wa kambi maalum ya siku tano inayoendelea katika Hospitali hiyo.
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Janeth Mmari
akimwelezea namna ya kujikinga na magonjwa ya moyo mkazi wa Chato aliyefika
katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na
matibabu ya moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano inayoendelea katika
Hospitali hiyo.
Wataalam wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao
wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) wakiwafanyia vipimo vya awali
wananchi waliofika katika Hospitali hiyo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na
matibabu ya moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano inayoendelea katika
Hospitali hiyo.
Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Geita wakiwa katika foleni ya kupatiwa
huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalum ya siku
tano inayofanywa na wataalam wa afya kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH).
Picha na: JKCI

Post a Comment

Previous Post Next Post