********
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) leo amefanya ziara ya kushtukiza katika eneo la Shule ya Msingi Sagani lililopandwa miti kwenye Maadhimisho ya Siku ya Upandaji Miti Kitaifa yaliyofanyika Machi 21, 2022 Wilayani Magu Mkoani Mwanza.
Lengo la ziara hiyo ni kuangalia maendeleo ya miti iliyopandwa na Wakala wa Huduma wa Misitu Tanzania (TFS) endapo inatunzwa vizuri au la.
Mhe. Masanja amemuagiza Mkuu wa Shule ya Msingi Sagani, Ruhumbika Kapesa, kuendelea kusimamia ukuaji wa miti hiyo ili ifikie lengo lililokusudiwa la kuifanya Wilaya ya Magu kuwa ya kijani