NAIBU WAZIRI CHILO AWATAKA WAVUVI KUTUNZA MAZINGIRA

 Na Robert Hokororo, Zanzibar


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis 

Hamza Chilo ametoa rai kwa wanufaika wa mradi wa boti za uvuvi 

zilizotolewa kupitia Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia

Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) kutofanya shughuli za kibinadamu zinazochangia 

uharibifu wa mazingira.


Ametoa rai hiyo leo Julai 20, 2022 wakati wa hafla ya makabidhiano ya boti sita 

za uvuvi zilizokabidhiwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na 

Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika Shehia 

ya Jongoe Kisiwa cha Tumbatu Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja, 

Zanzibar.


Mhe. Chilo alisema boti hizo zitumike kuleta katika tija katika mapambano ya 

athari za mabadiliko ya tabianchi zinazoikabili nchi yetu na duniani kwa ujumla, 

hivyo ni wajibu wa wanufaika wa mradi huo kuhakikisha wanatunza vyanzo vya 

maji, kufanya kilimo endelevu.


Alisema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais inaendeleza ushirikiano mzuri uliopo 

baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya 

Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na ndiyo maana inatekeleza miradi hii.


”Leo zinakabidhiwa boti hizi kwa vikundi vya wavuvi ambao ndio wanufaika 

wakuu kwa hiyo nitoe rai kwenu mtunze vyanzo vya maji ili viumbe vilivyomo 

navyo viweze kuishi kutunzwa na mazingira ndio kila kitu kwa vizazi vya sasa bna 

vijavyo,” alisema Chilo.


Aidha, Mradi wa EBARR ni wa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2018 hadi 2022 na unatekelezwa katika Wilaya za Mvomero (Morogoro), Simanjiro (Manyara), Kishapu (Shinyanga), Mpwapwa (Dodoma) Tanzania Bara na Kaskazini A - Unguja, upande wa Zanzibar. 


Maeneo ya Mradi yalichaguliwa kwa kuzingatia maeneo yenye ukame yenye jamii za wakulima, wafugaji, na wavuvi kwa lengo la kuongeza uwezo wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi katika jamii za vijijini kwa kuimarisha mifumo ikolojia na shughuli mbadala za kujiongezea kipato.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali 

Mwinyi akikabidhi boti sita za uvuvina vifaa vyake kwa kikundi cha wavuvi katika 

katika Shehia ya Jongoe Kisiwa cha Tumbatu Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa 

Kaskazini Unguja, Zanzibar leo Julai 20, 2022 kupitia Mradi wa Kuhimili 

Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) 

unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis 

Hamza Chilo akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya boti sita 

za uvuvi na vifaa vyake iliyofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  

Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika Shehia ya Jongoe Kisiwa 

cha Tumbatu Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar leo Julai 

20, 2022.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis 

Hamza Chilo akishiriki matukio mbalimbali wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar 

na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambaye 

alikabidhi boti sita za uvuvi kwa vikundi vya vya Shehia ya Jongoe Kisiwa cha 

Tumbatu Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar leo Julai 20, 

2022 kupitia Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo 

Ikolojia Vijijini (EBARR) unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais

Post a Comment

Previous Post Next Post