**********************
Dodoma 20 Julai, 2022.
Kufuatia Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumteua Jenerali (Mst) Venance Salvatory Mabeyo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) tarehe 30 Juni, 2022, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi H. Chana (Mb) kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 5(2) cha Sheria ya Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Sura ya 284 kikisomwa pamoja na Jedwali la Pili, Kipengele Na. 1 na 2(1)(b)-(c), amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi ya NCAA:-
- Bw. Benson Obdiel Kibonde, Mhifadhi Wanyamapori Mkuu (Mst) Pori la Akiba Selous.
- Bw. Bakari Nampenya Kalembo – Mshauri wa Masuala ya Fedha.
- Bibi Agnes Kisaka Meena, Mkurugenzi wa Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
- Prof. Esther William Dungumaro, Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu, Mkwawa (MUCE).
- Prof. Herrieth Godwin Mtae, Mtaalamu wa Maendeleo ya Uchumi wa Jamii, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).
- Prof. Henry Chalu, Profesa Mshiriki, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
- Bw. Simon Vedastus Ntobbi, Afisa Tawala Mkuu Daraja la I, Ofisi ya Rais – UTUMISHI.
Uteuzi huu ni wa miaka mitatu kuanzia tarehe 20 Julai, 2022 hadi 19 Julai, 2025.