AFISA MTENDAJI MKUU BRELA APONGEZA JITIHADA ZA WIPO KUENDELEZA UBUNIFU



                        .........................

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Godfrey Nyaisa amepongeza Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (WIPO) kwa jiihada linazozifanya za kuendeleza kazi za ubunifu kwa maendeleo ya  nchi wanachama. 

Pongezi hizo amezitoa wakati akiwasilisha taarifa ya nchi  kuhusu  Miliki Ubunifu na ushirikiano  kati ya Tanzania na WIPO  katika Mkutano Mkuu wa 63 wa Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (WIPO), unaofanyika Geneva Uswisi.

 Bw. Nyaisa  amesema  jitihada hizo  za kuendeleza kazi za ubunifu kwa maendeleo ya nchi wanachama, zitazaa matunda na kuendeleza bunifu mbambali na kuleta tija kwa nchi wanachama.

Ameeleza pia ushirikiano  kati ya Tanzania  na WIPO utalenga katika kusaidia wajasiriamali na vijana katika kutumia Miliki Ubunifu kwa maendeleo ya ubunifu.

 Mkutano  huo wa siku saba ulioanza tarehe 14 Julai, 2022,  unahudhuriwa pia na   Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Bishara na Mali,  (BPRA) Zanzibar, Bi. Mariam Mliwa Jecha, Mkuu wa Idara ya Uraghbishi wa Ushindani kutoka  Tume ya Ushindani (FCC) Bi. Magdalena  Utouh pamoja na Msajili Msaidizi Mkuu kutoka BRELA, Bi. Loy Mhando.

Post a Comment

Previous Post Next Post