WATUMISHI TANAPA WAHIMIZWA KUENDELEA KUTOA HUDUMA BORA KWA WATEJA




 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Francis Michael amewasisitiza watumishi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) wandeleee kutoa huduma Bora kwa wateja ili wafurahie safari zao wanapotembelea Tanzania.

Dkt. Francis amesema hayo alipotembelea Makao Makuu ya shirika hilo jijini Arusha kwa lengo la kukutana na kuzungumza na wafanyakazi wa taasisi hiyo.

Amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amefanya makubwa kupitia filamu ya Royal Tour Tanzania aliyoizindua jijini Arusha Aprili 28I2022.

“Watalii wengi watamiminika nchini ikiwa ni matokeo ya filamu hiyo, hivyo ni muhimu tujiandae katika kila nyanja, tumezindua filamu ya Royal Tour Tanzania, tutarajie wageni wengi kutembelea nchi yetu. Tujiandae kuwapa huduma nzuri” amesema Dkt. Francis.

Filamu ya Royal Tour Tanzania imezinduliwa jijini Arusha ikiwa ni mwendelezo wa shughuli ya uzinduzi wa filamu hiyo ulioanzia nchini Marekani katika jiji la New York na Los Angeles.

Awali, Kamishna wa Uhifadhi – TANAPA, William Mwakilema akitoa taarifa fupi kuhusu utendaji kazi wa Shirika alimweleza Katibu Mkuu kuwa Shirika limekuwa likipambana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya wananchi kuingiza mifugo ndani Hifadhi za Taifa jambo ambalo linatishia ustawi wa uhifadhi nchini.

Post a Comment

Previous Post Next Post