PMT yaendelea kuvuna wanamichezo wa OCR

Na Eben-Ezery Mende 

SHIRIKISHO la Michezo ya Pentathlon Tanzania (PMT) limeendelea kukusanya wanamchezo wa mbio xa vikwazo (OCR) katika mkakati wake wa kuhakikisha mchezo huo unatambulika na kuwa nyota kati ya michezo pendwa hapa nchini.

Akizungumza na kiongozi wa Habari na Mawasiliano wa OCR, Mtumishi wa Taasisi ya Sahara Ventures,  Amanzi Mpingo amesema ameona mchezo huo ukitangazwa kwenye vyombo vya habari akashawishika kujiunga.

Mpingo ameyasema hayo katika fukwe za Dengu jijini Dar es Salaam baada ya kushiriki mchezo huo na kujiridhisha kuwa ni mzuri na unaotakiwa kuchezwa kwa rika na jinsi zote.

Amesema ipo michezo mingi ambayo inachezwa kwa kuzingatia jinsi na rika (umri) lakini mchezo wa mbio za vikwazo umejipambanua vizuri kwamba unawashirikisha watoto, vijana, wanaume, wanawake na wazee.

"Ni nadra kuona mchezo wa kutobagua umri, huu wa mbio za vikwazo unawaweka watu karibu kwa makundi yote ukifanikiwa kueleweka hapa nchini utawanufaisha wachezaji lakini pia mashabiki", anasema Mpingo.

Nae Mkurugenzi wa Ufundi wa OCR, Bw. Joshua Kayombo (Joka) amesema utaratibu wa mchezo huo utaendelea kufanyika kila siku ya Jumamosi ili kuweka uelewa wa mchezo huo.

Joka amesema kila Mtanzania ambaye anapenda kushiriki mchezo huo anakaribishwa katika Fukwe za Dengu Jumamosi kuanzia saa 12:00 asubuhi na tamati ni saa 3;00 asubuhi.  .    Mwanamichezo Amanzi Mpingo



Post a Comment

Previous Post Next Post