PROF.MBARAWA AMEAGIZA JENGO LA STESHENI YA RELI YA KISASA DAR ES SALAAM-SGR LIKAMILISHWE KWA WAKATI

Mkurugenzi Mkuu wa TRC Mhandisi Masanja Kadogosa akimueleza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa (aliuevaa shati jeupe) maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Stesheni ya Reli ya Kisasa Dar es salaam-SGR.


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akifanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Stesheni ya Reli ya Kisasa Dar es salaam-SGR.

………………………

NA MUSSA KHALID

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa ameuagiza Uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa Jengo la Stesheni ya Reli ya Kisasa Dar es salaam-SGR kukamilika kwa wakati kabla ya mwezi wanne mwaka huu.

Waziri Prof.Mbarawa amesema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akifanya ziara ya kukagua maendeleo ya Shesheni hiyo akiwa ameambata na Mkurugenzi Mkuu wa TRC Mhandisi Masanja Kadogosa pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo.

Aidha Prof Mbarawa ametoa maelekezo kuwa jengo hilo limalizike kwa haraka  lakini pia litakapoanza kutumika liwekewe usimamizi mzuri ili lindelee kuwa katika ubora wake.

Amesema wakati umefika jengo hilo liweze kumalizika na sio kuahidi kili wakati hivyo mpaka mwezi wa nne mwaka huu ni vyema likakamilika.

Amesema pia Jengo hilo lifanyiwe ukarabati wa mara kwa mara ili liweze kukaa kwa muda mrefu na na hivyo kuonekana kuwa la mfano kwa wageni mbalimbali pamoja na wananchi pindi wanapolitembelea.

‘Hili jengo ni zuri sana kwani limejengwa kwa miundombinu mizuri hivyo ni lazima tuwe na utamaduni wa kuja kulisimamia vinginvyo miaka miwili au mitatu litakuwa halitamaniki lazima tubadilike’amesema Prof Mbarawa

Hata hivyo amewataka TRC kubadilika katika utoaji wa huduma wa SGR tofauti na treni ya zamani ili watu waone utofauti wa kuwa treni hiyo ni ya kisasa kwani kufanya hivyo watapata heshima kubwa kwa watanzania.

Post a Comment

Previous Post Next Post