CEO DAWASA Awaasa Watumishi Kuboresha Ufanisi Wa Kazi Kwa Kuwathamini Wateja Na Kudhibiti Upotevu Wa Maji

 Na Mwandishi Wetu

WATUMISHI wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), wametakiwa kuthamini kazi ya kutoa huduma ya Majisafi na usafi wa Mazingira kwa wateja na kuitenda kwa ufanisi mkubwa.

Akiongea katika kikao kazi cha wafanyakazi wote kilichofanyika hivi karibun, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja, amesema huduma ya maji ni huduma takatifu hivyo kila mtumishi anapaswa kufanya wajibu wake ma kwa uaminifu mkubwa.

"Sote tunapaswa kuelewa kwamba kufanya kazi katika Sekta ya maji ni kwa kusudi maalum na sio kwa bahati mbaya, hivyo kila mtumishi ana mchango sahihi katika kukuza maendeleo ya Mamlaka" alisema Mhandisi Luhemeja.

Ameongeza kuwa kila mtumishi wa Mamlaka analo jukumu la kutengeneza mazingira mazuri ya kuishi kwa wakazi wa Dar es Salaam na Pwani kupitia huduma ya majisafi kwa kuhakikisha upotevu wa maji unadhibitiwa ili kuboresha upatikanaji wa maji kwa wateja.

Amesema, kuwa udhibiti wa upotevu wa maji unasaidia Mamlaka kuokoa mapato yanayokosekana ya kuwezesha kuboresha huduma.

Kikao kazi hicho ni cha kwanza tangu kuanza Mwaka 2022 kilicholenga kufanya tathimini ya utendaji kwa mwaka uliopita.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), wakikagua mita ya mteja wao katika kampeni ya kukusanya madeni kwa wateja mbalimbali wa mamlaka hiyo katika jijini la Dar es Salaam.
Mfanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), akisoma mita ya mteja katika operesheni ya kukusanya madeni inayoendelea ambapo mamlaka hiyo imewataka wananchi kulipia huduma ya maji ili kuiwezesha kutoa huduma bora zaidi.

Post a Comment

Previous Post Next Post