TBS IMEADHIMISHA SIKU YA VIWANGO AFRIKA KWA KUKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA SHINDANO LA INSHA

        

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw.David Ndibalema (Kulia) akiwakabidhi hundi na vyeti washindi 10 wa shindano la Insha katika Maadhimisho ya Siku ya Viwango Afrika ikiyofanyika makao makuu ya shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam. 

Washindi 10 wa shindano la insha wakijitambulisha katika hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Viwango Afrika ikiyofanyika makao makuu ya shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.Washindi 10 wa shindano la Insha wakipata picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw.David Ndibalema katika hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Viwango Afrika ikiyofanyika makao makuu ya shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.

***************************

NA MWANDISHI WETU

Viwango vinapokuwa vimekamilishwa na kupitishwa na mamlaka husika, huweka mainisho na misingi muhimu ya kuzingatia katika uzalishaji wa bidha, utoaji huduma katika maeneo mbalimbali ya jamii na utendaji katika sekta mbalimbali ikiwemo sanaa,utamaduni na maeneo ya urithi.

Ameyasema hayo leo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw.David Ndibalema kwenye hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Viwango Afrika ikiyofanyika makao makuu ya shirika hilo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo Bw.Ndibalema amesema kuwa matakwa ya viwango yanazingatia kuwezesha kutolewa kwa bidhaa na huduma bora kwa jamii husika hivyo kulinda afya,usalama na mazingira na hatimaye kuchangia katika uchumi endelevu wa taifa.

“Ni wazi kuwa iwapo utaratibu wa kuandaa viwango utahusisha jamii kisha matakwa yake yakazingatiwa katika nyanja zote husika, viwango vitakuwa na mchango mkubwa katika mapambano dhidi ya changamoto zinazokabili sekta ya sanaa, utamaduni na urithi wetu”. Amesema Bw.Ndibalema.

Aidha, Bw.Ndibalema amesema upo utofauti mkubwa katika kukuza uchumi bunifu kwenye sekta ya sanaa utamaduni na urithi wa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania ukilinganisha na nchi zinazoendelea kwa sababu ya changamoto mbalimbali ikiwemo miundombinu, biashara, fedha na matumizi ya viwango.

Pamoja na hayo Bw.Ndibalema amewapongeza waandaji wa shindano la isha kwani ushirikishwaji wa wanachuo ninnjia mojawapo ya kueneza uelewa kuhusiana na matumizi ya viwango katika bidhaa na huduma mbalimbali.

Vyuo vilivyoshiriki katika shindano la isha ni vyuo 32 ambapo washindi 10 wamepatika kutoka vyuo hivyo na kukabidhiwa zawadi.

Post a Comment

Previous Post Next Post