Na. John Mapepele
Watoa mada mbalimbali kwenye kongamano la kuelezea mafanikio ya michezo wametoa shuhuda na kupongeza mageuzi na mapinduzi makubwa huku wakisema mama Samia ameupiga mwingi na kuondoka nao.
Aliyeanza ni Katibu Mkuu. Dkt, Hassan Abbasi ambaye amesema Mhe. Rais amekuwa na utashi wa kisiasa kwenye michezo, amefanya uwekezaji mkubwa na kuboresha na kujenga miundombinu za michezo.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa watu wenye Ulemavu (TAFF) Peter Sarungi amefafanua kuwa kutokana na maono makubwa ya Mhe. Rais timu yao imefuzu kwenda kombe la dunia.
Aidha, ameongeza kuwa kutokana na utashi huo Mhe. Rais amefungua ajira kubwa za kitaifa na kimataifa kwa wachezaji walemavu.
Amesema hadi sasa wachezaji wanne (4) wameshapata timu katika mataifa mbalimbali duniani.
Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Jackson Ndaweka amesema mashindano ya taifa ya riadha yameweza kufanyika kwa mafanikio makubwa.
"Tunashukuru sana mama sasa tumeanza kupata udhamini kwa mashindano yetu kutoka katika mashirika ya Serikali"