SEKTA YA UJENZI YAKUTANA NA KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU

 


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Selemani Kakoso (Mb), akisisitiza jambo wa Uongozi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) walipowasilisha makadirio ya bajeti ya sekta hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2022/23, Bungeni jijini Dodoma. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi anaesimamia Sekta ya Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya na Kaimu Katibu Mkuu Sekta ya Ujenzi Richard Mkumbo.Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Mhandisi Godfrey Kasekenya, akiwasilisha makadirio ya bajeti ya Sekta ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha wa 2022/23, kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Bungeni jijini Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Selemani Kakoso (Mb) na kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Sekta ya Ujenzi Richard Mkumbo.Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakifuatilia uwasilishwaji wa makadirio ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), kwa mwaka wa fedha wa 2022/23, yaliyowasilishwa na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Mhandisi Godfrey Kasekenya (hayupo pichani), Bungeni jijini Dodoma.Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Richard Mkumbo, akifafanua jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakati wa kuwasilisha makadirio ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) kwa mwaka wa fedha wa 2022/23, Bungeni jijini Dodoma. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Selemani Kakoso (Mb)Mtendanji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Daud Kondoro, akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, katika kikao cha makadirio ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), kwa mwaka wa fedha wa 2022/23, yaliyowasilishwa kwa wajumbe wa kamati hiyo, Bungeni jijini Dodoma.Baadhi ya Watendaji kutoka taasisi mbalimbali za Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), wakifuatilia uwasilishwaji wa makadirio ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), kwa mwaka wa fedha wa 2022/23, iliyowasilishwa na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya (hayupo pichani), mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Bungeni jijini Dodoma. Picha na WUU

Post a Comment

Previous Post Next Post