WAZIRI JAFO ATOA MIEZI MIWILI KWA KAMPUNI YA DCG KUFANYA MCHAKATO WA ATHARI YA MAZINGIRA

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo wa pili kutoka kulia akitoa maelekezo kwa mmoja wa wasimamizi wa kampuni ya Dsm Corridor Group(DCG) inayojihusisha na uingizaji wa kemikali ya Salpha katika ghala la kuhifadhia kemikali hiyo kwenye bandari kuu ya Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wasimamizi wa kampuni ya Dsm Corridor Group (DCG)namna wanavyosimamia kemikali ya Sulphur kuzuia isiharibu mazingira kwenye bandari Kuu ya Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo mwenye suti, akiwa na wataalamu wa mazingira kutoka NEMC pamoja na wataalamu kutoka Ofisi ya mkemia Mkuu wa Serikali kwenye ziara ya kukagua kemikali ya salpha iliyoingizwa Nchi kama inazingatia uhifadhi wa Mazingira kwenye bandari kuu ya Dar es Salaam.

Ghala linalohifadhi kemikali ya Salpha aliloembelea Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo hayupo pichani. Waziri Jafo alifanya ziara kwenye ghala hilo kujiridhisha na utunzaji wa mazingira wakati wa shughuli za utunzaji na usafirishaji wa kemikali hiyo, kwenye bandari kuu Jijini Dar es Salaam.

……………………………………………………………

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo, ametoa miezi miwili kwa kampuni ya DSM Corridor Group Limited (DCG) kukamilisha mchakato wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira(TAM) ili kuweza kuepuka athari za kimazingira  zitakazotokana na uingizwaji wa kemikali ya salfa katika bandari ya Dar es Salaam. 

Ameyasema hayo alipofanya ziara ya ukaguzi wa mazingira katika Bandari ya Dar es Salaam, ili kuweza kujionea namna ya uhifadhi wa kemikali  zinazoingizwa nchini kupitia bandari ya Tanzania chini ya Kampuni ya usafirisahji ya DCG na kuelekea nchi jirani ya Burundi, hata hivyo ameitaka kampuni hiyo kuchagua mshauri elekezi wa mazingira mwenye sifa kulingana na taaluma aliyonayo ili shuguli hizo zifanyike bila ya kuathiri mazingira.

 Aidha Mhe. Jafo amesema kuwa tunapenda uwekezaji lakini wazingatie utunzaji wa mazingira kwa ajili ya kujenga uchumi wa kati kwa wananchi wenye afya bora. Amesema kuwa kitendo cha kampuni hiyo kuingiza kemikali hizo Nchini na kupeleka Nchi jirani inaonyesha ni dhahiri kuwa Uchumi wa Nchi Unakuwa kwa namna moja au vingine hivyo amewataka uhifadhi wake uwe mzuri ili kuweza kuhifadhi na kutunza mazingira yetu.

“Nimefurahishwa mzigo wa kemikali ya salfa ni ile ya chembechembe na sio ya unga kama tunavyofahamu Salfa ya unga inaathari kubwa ya kimazingira kuliko ya chembechembe, hivyo nimeshauri waendelee kuingiza kemikali ya salfa ya chembechembe ili kuepusha madhara ya kimazingira. Ninachotaka mfanye kazi kwa uadilifu hii salfa inaenda nchi jirani lazima tuwaaminishe kuwa watanzania tunaweza kufanya kazi huku mazingira yetu yakiwa salama na mazuri.”

Kwa upande wake Bwana Thobias Mwesiga Afisa Mwandamizi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), amesema kuwa swala la kemikali lipo chini ya mkemia mkuu wa serikali lakini NEMC wamekuja kukagua katika kusimamia masuala la kimazingira hasa wakati wa ushushwaji na uhifadhi wa kemikali hizo zisiweze kuingia kwenye maji au udongo na kuathiri viumbe vilivyopo kwenye maji na aridhini. 

Vile vile Msimamizi wa kitengo cha ukaguzi kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kanda ya Mashariki Bwana Jeremiah Nkurukuru, amesema kuwa wameshirikiana na kampuni ya DCG katika kuhakikisha wanawapa muongozo ambao watahifadhi kemikali hizo bila ya kuathiri mazingira na binadamu kuwa salama. Ameendelea kusema kuwa wataendelea kuwapa muongozo na bado kuna wakaguzi wapo wanaendelea kusimamia zoezi

Post a Comment

Previous Post Next Post