TANESCO YACHANGIA MILIONI 20 MATIBABU YA WATOTO WENYE KIBIONGO MOI

 

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Tulia Ackson akipokea mfano wa Hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 20 kutoka kwa Bi. Johari Kachwamba Mkuu wa Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO  ambazo shirika hilo limechangia kwa ajili ya matibabu ya watoto wenye Kibiongo katika Hospitali ya MOI Muhimbili jijini Dar es salaam wakati wa mbio za marathon kilomita 21,10 na kilomita 5 zilizofanyika kwa ajili ya kuchangia matibabu ya watoto 40 wenye Kibiongo kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi MOI Profesa Charles Anael Mkonyi na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt.Respicious Boniface.

(PICHA NA JOHN BUKUKU-DAR ES SALAAM)

…………………………………….

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limechangia kiasi cha Shilingi Milioni Ishirini kwa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), ili kusaidia na kuwezesha matibabu ya watoto wenye vibiongo katika hospitali hiyo.

Akiongea katika Mbio fupi za kuchangia matibabu hayo (Moi marathoni) Juni 27,2021, katika viwanja vya chuo cha udaktari Muhimbili MUHAS, Meneja uhusiano wa TANESCO, Bi. Johary Kachwamba amesema kuwa TANESCO imeona umuhimu wa kurudisha kwa jamii sehemu ya kile inachokipata kupitia mauzo ya Umeme kwa kusaidia matibabu ya watoto hao.

“TANESCO imeamua kuangaza maisha ya jamii yetu kwa namna ya tofauti, tunafarijika kwamba matibabu haya yataokao uhai na kurejesha furaha kwa watoto wenye vibiongo” amesema Bi. Kachwamba

Sambamba na kuchangia kiasi hicho, wafanyakazi wa TANESCO pia wameshiriki katika kukimbia mbio hizo katika makundi ya km 5, Km 10 na Km 21, ambapo mshindi wa tatu mbio za Km 5, kwa upande wa Wanaume ni Bw. Sebastian Kwayu, kutoka TANESCO.

Mgeni Rasmi aliepoke hundi kwa niaba ya MOI katika tukio hilo ni, Mhe. Tulia Akson, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo alitoa shukrani kwa wote waliochangia ikiwa ni pamoja na TANESCO.

Akizungumza mara baada ya kushiriki mbio hizo za MOI Marathon  Sebastian Kwayu ambaye ni afisa Mkuu Ustawi TANESCO aliyeshiriki katika mbio za Km 5 na kushika nafasi ya tatu ameshukuru kwa kushika nafasi ya tatu katika mbio hizo kwakuwa ushindi huo unampa hamasa ya kuendelea kushiriki mbio hizo.

Amesema kama mwajiriwa na Shirika la Umeme Tanzania anajisikia fahari kwa Shirika lao kuchangia matibabu hayo kwa sababu yataenda kuokoa maisha ya watoto wenye matatizo ya kibiongo jambo ambalo litawapa faraja watoto hao wenye matatizo.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Tulia Ackson akipokea mfano wa Hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 20 kutoka kwa Bi. Johari Kachwamba  Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO  ambazo shirika hilo limechangia kwa ajili ya matibabu ya watoto wenye Kibyongo katika Hospitali ya MOI Muhimbili jijini Dar es salaam wakati wa mbio za marathon kilomita 21,10 na kilomita 5 zilizofanyika kwa ajili ya kuchangia matibabu ya watoto 40 wenye Kibyongo kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi MOI Profesa Charles Anael Mkonyi na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji na Baadhi ya wakuu wa vitengo.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Tulia Ackson akimkabidhi cheti Bi. Johari Kachwamba Mkuu wa Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO  mara baada ya wafanyakazi wa shirika hilo kuchangia   matibabu ya watoto wenye Kibyongo katika Hospitali ya MOI Muhimbili jijini Dar es salaam wakati wa mbio za MOI marathon kilomita 21,10 na kilomita 5 zilizofanyika kwa ajili ya kuchangia matibabu ya watoto 40 wenye Kibyongo kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi MOI Profesa Charles Anael Mkonyi na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji

Marathon  Sebastian Kwayu ambaye ni afisa Mkuu Ustawi TANESCO aliyeshiriki katika mbio za Km 5 na kushika nafasi ya tatu akiwa katika picha ya pamoja na mshiriki mwenzake.

 

Bi. Johari Kachwamba Mkuu wa Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kulia na Elizaberth Mramba Mtangazaji wa TBC wakishiriki mazoezi mara baada ya kushiriki mbio hizo.

Bi. Johari Kachwamba Mkuu wa Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kulia na Elizaberth Mramba Mtangazaji wa TBC  na wadau wengine wakishiriki mazoezi mara baada ya kushiriki mbio hizo.

Picha mbalimbali zikionesha baadhi ya wafanyakazi wa shirika la umeme la Tanzania TANESCO wakishiriki katika mazoezi ya viungo kabla ya kuanza kwa mbio za Km 5 katika mbio za MOI Maraton.

   

Post a Comment

Previous Post Next Post