RC MALIMA AWATUMIA SALAMU WANAOSAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU, WANAOPITISHA DAWA ZA KULEVYA TANGA ,AWAAMBIA WASIJARIBU

 

MKUU
wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akizungumza na waandishi wa habari ofisini
kwake kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari

MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima amewatumia salamu
mawakala wa wahamiaji haramu ambao wanatumia mkoa huo kuwapitisha na wale
wanaopitisha dawa za kulevya kwamba wasijaribu kufanya hivyo maana
watakachokutana nacho kitakuwa historia kwao.

RC Malima aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa
habari mkoani Tanga ambapo alisema mkoa huo hautakuwa dezo ya kupitisha wahamiaji
haramu na kama kuna watu wanadhani anatania wafanye hivyo waone watakumbana na
jambo gani.

Alisema kwamba mkoa huo hautakuwa sehemu ya watu kupitisha
mauzauza yao na wasijaribu kutokana na kwamba wamejipanga vilivyo kuhakikisha
vitendo vya namna hiyo havifanyika kwenye mkoa huo huku akitoa onyo kwa
wanaodhani wanaweza kujaribu.

“Ndani ya wiki mbili wahamiaji haramu wameongezeka naomba
wasiufanye mkoa wa Tanga kuwa ni dezo ya wao kupitia na niwaambie kwamba Tanga
hautakuwa mkoa wa kupitisha mauzauza yao na hata wale ambao wanafikiria kwamba
wanaweza kupitisha dawa za kulevya wasijaribu zari kwani tumejipanga kuwashughulikia”Alisema

Alisema wahamiaji haramu hao wanapitia mkoa wa Tanga kwenda
mikoa ya Pwani ,Dar,Bagamoyo kwa hiyo aliwataka waandishi wa habari kufikisha
salama kwa wananchi kwa wale wanaojua wazi kwamba watu wanao wanashirikiana kwenye
kusafirisha binadamu wanaowatoa mkinga wanawasafarisha usiku kwa usiku.

“Hao watu ambao wanao wanashiriikiana kusafrisha binadamu
wanawatoa wilaya ya Mkinga kuwasafirisha usiku kwa usiku  wengine wanapita Korogwe wanatoka Kilindi
wanachana Korogwe hadi Handeni wanapitia Mkata wanaingia Pwani wengine wanatokea
Mvomero pia eneo la Gairo hilo ni tatizo kubwa na hawawezi kufanikiwa kama
hawana watu ambao wana shirikishiana nao”Alisema

Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka waandishi wa habari mkoa wa
Tanga wafikishe ujumbe kwamba wale wanaotumika kuwasafirisha huenda dhambi ya
kusafirisha ni kubwa sana kuliko kusafirishwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post