WAZIRI NDUMBARO AKAA KIKAO KAZI NA WADAU WA SEKTA YA UTALII

 

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi  wakimsikiliza  Balozi wa Umoja wa  Falme za Kiarabu (UAE), Mhe. Khalifa Abdulrahman Almazrzouqi wakati wa  kikao kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambapo wamezungumzia mikakati ya kukuza Utalii nchini ikiwemo kutangaza vivutio vya Utalii vilivyopo nchini katika ndege za Emirates na  vyombo vya habari vya kimkakati vilivyopo Uarabuni ili kuteka soko la Utalii katika Umoja wa Falme hizo. 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro   akimsikiliza  Balozi wa Umoja wa  Falme za Kiarabu (UAE), Mhe. Khalifa Abdulrahman Almazrzouqi kbala ya kuagana mara baada ya kumaliza kikao kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaa ambapo wamezungumzia mikakati ya kukuza Utalii nchini ikiwemo kutangaza vivutio vya Utalii vilivyopo nchini katika ndege za Emirates na  vyombo vya habari vya kimkakati vilivyopo Uarabuni ili kuteka soko la Utalii katika Umoja wa Falme hizo. 

Waziri wa Maliasil na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na Menejimenti ya NMB makao makuu  katika kikao kilichofanyika leo mapema Jijini Dar es Salaam kilicholenga kuboresha mahusiano kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Benki hiyo ili kufanya kazi kwa pamoja  katika kutangaza vivutio vya utalii nchini kwa kuwawezesha kufanya malipo kupitia Benki hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post