WAZIRI NDUMBARO AZINDUA NAMBA MAALUM NA KUKABIDHI SIMU 14 KWA MAMLAKA ZA MALIASILI NA UTALII

 

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dkt Damas Ndumbaro,akizindua  namba maalum na kukabidhi simu 14 ikiwa ni huduma ya mawasiliano ya bure kwa wananchi ili waweze kupiga simu Mamlaka za Maliasili na Utalii pindi wanapovamiwa na wanyama hatari hafla hiyo imefanyika leo Mei 27,2021 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dkt Damas Ndumbaro,akizungumza moja kwa moja na mwananchi wa Mvomero Mkoani Morogoro ambaye ameripoti taarifa za kuvamiwa kwa tembo ambao wameharibu mazao yake leo Mei 27,2021 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dkt Damas Ndumbaro,akimakbaidhi simu 4 Naibu Kamishna wa Uhifadhi TANAPA Bw.William Mwakilema ambazo zitakazowawezesha wananchi  kupiga simu bure kwa Mamlaka za Maliasili na Utalii pindi wanapovamiwa na wanyama hatari zoezi lililofanyika leo Mei 27,2021 jijini Dodoma.Kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja.

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dkt Damas Ndumbaro,akimakbaidhi simu 1 Kamishna wa Uhifadhi NCAA Dkt.Freddy Manongi itakayotumika kuwawezesha wananchi  kupiga simu bure kwa Mamlaka za Maliasili na Utalii pindi wanapovamiwa na wanyama hatari zoezi lililofanyika leo Mei 27,2021 jijini Dodoma.Kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja.

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dkt Damas Ndumbaro,akizungumza mara baada ya kuzindua namba maalum na kukabidhi simu 14 ambazo zitamuwezesha mwananchi kupiga simu bure kwa Mamlaka za Maliasili na Utalii pindi wanapovamiwa na wanyama hatari leo Mei 27,2021 jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja,akizungumza mara baada ya kuzindua namba maalum na kukabidhi simu 14 ambazo zitamuwezesha mwananchi kupiga simu bure kwa Mamlaka za Maliasili na Utalii pindi wanapovamiwa na wanyama hatari leo Mei 27,2021 jijini Dodoma.

 Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi,akizungumza mara baada ya kuzindua namba maalum na kukabidhi simu 14 ambazo zitamuwezesha mwananchi kupiga simu bure kwa Mamlaka za Maliasili na Utalii pindi wanapovamiwa na wanyama hatari leo Mei 27,2021 jijini Dodoma.

……………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dkt Damas Ndumbaro,amezindua namba maalum na kukabidhi simu (14) zitakazo wawezesha wananchi kupiga simu bure kwa mamlaka mbalimbali za maliasili na utalii kwa ajili ya kutoa taarifa za matukio ya wanyama wakali na waharibifu wanaovamia katika maeneo yao.

Akizungumza leo Mei 27,2021 jijini Dodoma wakati wa kukabidhi  simu 14 kwa Maafisa wa uhifadhi amesema  kuwa hiyo yote ni katika kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambavyo imeelekeza kuwekea kwa mikakati ya kupunguza migogoro kati ya wananchi na wanyama .

Dkt.Ndumbari  amekabidhi simu katika Taasisi za uhifadhi ikiwemo TANAPA,TAWA,NCAA mpoja ikibaki Wizarani ambapo amesema namba hizo ni bure itawasaidia wananchi kutoa taarifa juu ya madhara ya tembo wanapoingia katika Makazi yao.

“Hii itasaidia watanzania wanyonge na simu watapiga bure kwa mamlaka mbalimbali zinazohusika na Maliasili na Utalii kwa ajili ya kutoa taarifa za matukio ya kuvamiwa na   wanyama wakali, utaratibu huu pia Utasaidia kufikisha taarifa kwa haraka kwenye vituo vya utendaji” amesema Ndumbaro

Dkt Damas Ndumbaro amesema utaratibu huo mpya utasaidia kupata taarifa kwa haraka katika kituo cha karibu hasa pindi tuko la uvamizi wa wanyama wakali kama tembo linapotokea katika maeneo yao.

Katika uzinduzi huo pia Waziri Ndumbaro amezungumza moja kwa moja na mwananchi wa Mvomero Mkoani Morogoro ambaye ameripoti taarifa za kuvamiwa kwa tembo ambao wameharibu mazao yake.

Naye Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Mary Masanja amesema kuwa wananchi wamekuwa wakipatwa na madhara kwa kuvamiwa na wanyama wakali na waharibifu huku wengine wakipata Ulemavu,Vifo kadhaa lakini namba hizo za simu bure zitakuwa ni mkombozi kwa wananchi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara hiyo Dkt Allan Kijazi amesema changamoto ya wananchi kuvamiwa na wanyama hao wakali imekuwa ya muda mrefu licha ya jitihada tatizo kubwa kulikuwa ni Mawasiliano.

Post a Comment

Previous Post Next Post