PROF.MKUMBO AFURAHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA TBS

 Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) leo Jijini Dar es Salaam.Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya.

(PICHA NA EMMANUEL MBATILO)

*******************************

NA EMMANUEL MBATILO

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wamekuwa wakijitahidi kuhakikisha bidhaa zote zinazoingia kutoka nje na ambazo zinazalishwa hapa nchini zinakuwa na kiwango na ubora ambao unakubalika.

Ameyasema hayo Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo alipotembelea Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TBS, Prof.Mkumbo amesema kuwa wao kama Wizara wanaridhika na utendaji kazi wa shirika hilo kwani linatekeleza majukumu yake vizuri .

“Nimewakumbusha waongeze bidii katika kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa ubora ule ule lakini kwa spidi kubwa zaidi ili wafanyabiashara wanaofanya nao kazi waweze kupewa huduma mapema iwezekanavyo”. Amesema Prof.Mkumbo.

Aidha Prof.Mkumbo amesema kuwa TBS imekuwa haina bodi ya wakurugenzi na majukumu yake kwa mujibu wa sheria yamekuwa yakifanywa na Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara hivyo hilo jukumu lao kama serikali na amelichukua na watalifanyia kazi mapema ili bodi ya TBS iweze kuwepo na kuendelea kufanya kazi vizurikwa niaba ya Serikali

Post a Comment

Previous Post Next Post