KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI YAIAGIZA REA KUWAUNGANISHIA UMEME KWA WAKATI WATEJA WOTE WALIOLIPIA GHARAMA ZA KUUNGANISHIWA UMEME.

 Na Dorina G. Makaya - Iringa

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, imeitaka REA kusimamia na kuhakikisha Wateja wote waliolipia gharama za kuunganishiwa umeme, wanaunganishiwa umeme kwa wakati.

Maagizo hayo yametolewa tarehe 02 Mei, 2021 na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka (Mb) alipokuwa akizungumza na watendaji wa REA  kuhusu Miradi ya kusambaza umeme vijijini Mkoani Iringa kufuatia ziara ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali mkoani humo.

Mhe. Kaboyoka, ameiagiza REA kuhakikisha inaisimamia vizuri Miradi ya Kusambaza Umeme Vijijini ili kuepuka kuwa na Wigo wa nyongeza wakati wa utekelezaji wa Miradi au ‘Variations”.

Ameitaka REA kuhakikisha kuwa vifaa vinavyobaki kwa ajili ya kuwaunganishia wateja umeme mara Mradi unapokamilika, vikabidhiwe TANESCO na kuwataka TANESCO wavitumie vifaa hivyo kuwaunganishia wateja waliokuwa wamepangwa kwenye mkataba.

Aidha, mwenyekiti  huyo wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, ameitaka REA kuhakikisha kuwa, vitongoji ambavyo havijapatiwa umeme, chini ya Miradi ya REA III Mzunguko wa Kwanza, vinapatiwa umeme kupitia Mradi wa Ujazilizi “ Densification”.

Akizungumza kufuatia Maelekezo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Stephen Byabato (Mb.) ameiahidi  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuwa, Wizara ya Nishati itaendelea kusimamia taasisi ya REA na TANESCO ili kuhakikisha miradi yote ya umeme inatekelezwa kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa.

Amesema, Wizara ya Nishati itahakikisha wateja wote waliolengwa kupatiwa umeme wanapatiwa huduma hiyo kwa wakati na kwa gharama ya elfu 27,000/= tu.

Naibu Waziri Byabato  amekumbushia kuwa, miradi ya umeme vijijini inalenga kutoa huduma kwa wananchi ili kuwawezesha kufanya shughuli za kiuchumi ili kujiongezea kipato.

Vile vile, Naibu Waziri Byabato, amewaeleza wananchi wa kijiji cha Holo na wengine kote nchini, endapo watakutana na changamoto yoyote kuhusu suala la kuunganishiwa umeme ama kutakiwa kulipa zaidi ya Shilingi 27,000/=, wawasiliane na Mameneja wa TANESCO wa ngazi za wilaya na Mikoa ili washughulikie changamoto hizo mara moja.

Naye, Mkurugenzi  Mkuu wa REA, Mha. Amos Maganga amesema, amepokea maelekezo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu  za Serikali na ameahidi kuyafanyia kazi ipasavyo maelekezo hayo.

Katika Mradi wa REA III Round ya 1, jumla ya vijiji vilivyopatiwa umeme ni vijiji 42 kati ya  vijiji 42 vilivyopangiwa kuunganishiwa umeme katika Wilaya ya Iringa Vijijini. Pia, Jumla ya watejwa 1,775 kati ya 1,585 waliokua wamepangwa kuunganishiwa umeme katika Wilaya ya Iringa Vijijini wameunganishiwa umeme. Aidha, Gharama iliyotumika kwa wilaya nzima ya Iringa Vijijini ni Shilingi  16,678,715,788.00.

Katika kijiji cha Holo, jumla ya transfoma zilizofungwa ni tranfoma 1 kati ya 1 zilizokua zimepangwa na watejwa 42 kati ya 19 waliokuwa wamepangwa kuunganishiwa umeme, wameunganishiwa umeme, ambapo jumla ya shilingi 400,252,000.00 zimetumika kupeleka umeme kwenye kijiji cha Holo.

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Stephen Byabato (Mb.) akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu utekelezaji wa Miradi ya REA mkoani Iringa, kufuatia ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) mkoani Iringa tarehe 02 Mei, 2021 kuhusu Miradi ya kusambaza umeme mkoani humo. Kushoto kwa Naibu Waziri Byabato, ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka (Mb.)

Mwenyekiti wa Bodi ya REA. Wakili Julius Kalolo, Akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu utekelezaji wa Miradi ya REA mkoani Iringa, kufuatia ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) mkoani Iringa kuhusu Miradi ya kusambaza umeme mkoani humo. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Stephen Byabato (Mb.) na kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mha. Amos Maganga

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali wakiwa katika chumba cha mkutano kufuatia ziara yao kuhusu utekelezaji wa Miradi ya kusambaza umeme mkoani mkoani Iringa, tarehe 02 Mei, 2021.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka (Mb.) akizungumza na wanakijiji cha Holo kata ya Nyang’olo, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa (Hawamo pichani) tarehe 02 Mei, 2021 kuhusu suala la kuunganishiwa umeme kijijini hapo. Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Mhe. Richard Kasesela.

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Stephen Byabato (Mb.) akizungumza na wanakijiji cha Holo kata ya Nyang’olo, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa (Hawamo pichani) tarehe 02 Mei, 2021 kuhusu suala la kuunganishiwa umeme kijijini hapo. (Aliyesimama kushoto kwake) ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Mhe. Richard Kasesela.

Wananchi wa kijiji cha Holo kata ya Nyang’olo, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa) wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka (Mb.) (Hayumo pichani) wakati wajumbe wa Kamati hiyo walipowatembelea kijijini hapo kuhusu suala la kuunganishiwa umeme tarehe 02 Mei, 2021.

Wananchi wa kijiji cha Holo kata ya Nyang’olo, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Stephen Byabato, (Mb.) (Hayumo pichani) wakati wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, walipowatembelea kijijini hapo kuhusu suala la kuunganishiwa umeme tarehe 02 Mei, 2021.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka (Mb.) akizungumza na wanakijiji cha Holo kata ya Nyang’olo, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa (Hawamo pichani) tarehe 02 Mei, 2021 kuhusu suala la kuunganishiwa umeme kijijini hapo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka (Mb.) akizungumza na wanakijiji cha Holo kata ya Nyang’olo, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa (Hawamo pichani) tarehe 02 Mei, 2021 kuhusu suala la kuunganishiwa umeme kijijini hapo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka (Mb.) akisikiliza kero kuhusu suala la kuunganishiwa umeme kutoka kwa mmoja wa wanakijiji cha Holo kata ya Nyang’olo, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa tarehe 02 Mei, 2021.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe. Japhet Hasunga (Mb.) akizungumza na wanakijiji cha Holo kata ya Nyang’olo, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa (Hawamo pichani) tarehe 02 Mei, 2021 kuhusu suala la kuunganishiwa umeme kijijini hapo.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali wakifurahia jambo wakati wa mkutano wao na wanakijiji cha Holo kata ya Nyang’olo, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa (Hawamo pichani) tarehe 02 Mei, 2021 kuhusu suala la kuunganishiwa umeme kijijini hapo.

Baadhi ya Maafisa wa REA na TANESCO wakifuatilia Mkutano baina ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali na wanakijiji cha Holo kata ya Nyang’olo, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa uliofanyika tarehe 02 Mei, 2021 kuhusu suala la kuunganishiwa umeme kijijini hapo.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali walipokuwa wakiwasili Mkoani Iringa kwa ajili ya kufuatilia kuhusu Miradi ya Kusambaza umeme vijijini mkoani Iringa.

Post a Comment

Previous Post Next Post