MAKATIBU WAKUU OFISI YA MAKAMU WA RAIS WATEMBELEA MIRADI PEMBA

 

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Ngelela Maganga (wa tatu kushoto) akiwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu Bw. Mohammed Khamis Abdulla (kulia) wakiwa katika ziara ya kutembelea soko la samaki Tumbe ambalo kupitia Mradi wa Uvuvi na Maendeleo Shirikishi Kusini Magharibi ya Bahari ya Hindi (SWIOFish) lililopo Mkoa wa Kusini walipofanya ziara Pemba.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Ngelela Maganga (wa tatu kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalamu wa uvuvi wakati wa ziara ya kutembelea soko la samaki Tumbe ambalo kupitia Mradi wa Uvuvi na Maendeleo Shirikishi Kusini Magharibi ya Bahari ya Hindi (SWIOFish) lililopo Mkoa wa Kusini walipofanya ziara Pemba.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Ngelela Maganga na Naibu Katibu Mkuu Bw. Mohammed Khamis Abdulla wakiwa katika picha ya pamoja na wataalamu kutoka Wizara ya Uvuvi ya Zanzibar na wavuvi katika soko la samaki Tumbe ambalo kupitia Mradi wa Uvuvi na Maendeleo Shirikishi Kusini Magharibi ya Bahari ya Hindi (SWIOFish) lililopo Mkoa wa Kusini walipofanya ziara Pemba.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Ngelela Maganga (wa tatu kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalamu wa kilimo wakati wa ziara ya kutembelea bonde la mpunga la Ole lililopo Mkoa wa Kusini kupitia Mradi wa Kuongeza Tija na Uzalishaji wa Mpunga (ERPP) alipofanya ziara Pemba.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Ngelela Maganga akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Mhe. Mattar Zahour Masoud alipomtembelea ofisini kwake kabla ya kuanza ziara ya kutembelea bonde la mpunga la Ole lililopo Mkoa wa Kusini kupitia Mradi wa Kuongeza Tija na Uzalishaji wa Mpunga (ERPP).

Sehemu ya bonde la mpunga la Ole lililopo Mkoa wa Kusini kupitia Mradi wa Kuongeza Tija na Uzalishaji wa Mpunga (ERPP) ambalo limetembelewa na ujumbe wa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Ngelela Maganga.

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Mhe. Salama Mbarouk Khatib akitoa neno la shukrani kwa ujumbe wa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Ngelela Maganga uliofanya ziara katika mkoa huo wilayani Wete kwa ajili ya kutembelea soko la samaki Tumbe ambalo kupitia Mradi wa Uvuvi na Maendeleo Shirikishi Kusini Magharibi ya Bahari ya Hindi (SWIOFish).

Post a Comment

Previous Post Next Post