WAZIRI JAFO ARIDHISHWA MIRADI YA MUUNGANO

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akizungumza na mtumishi katika kituo cha afya cha Kianga kilichojengwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) lililopo mkoa wa Magharibi Zanzibar wakati wa ziara ya kikazi kukagua miradi inayotekelezwa pande mbili za Muungano.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akizungumza na wafanyabiashara na wananchi aliowakuta katika soko la Kinyasini lililojengwa kupitia mradi wa MIVARF lililopo katika mkoa wa Kaskazini wakati wa ziara ya kikazi kukagua miradi inayotekelezwa pande mbili za Muungano.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akikagua mojawapo ya vyumba vya madarasa katika skuli ya Mahonda ambao ni mradi wa TASAF.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akizungumza na wanafunzi wa skuli ya Fujoni iliyopo mkoa wa magharibi baada ya kukagua ujenzi wa ukumbi wa mitihani uliotekelezwa kupitia TASAF ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamad Hassan Chande akizungumza na wanafunzi katika skuli ya Fujoni iliyopo mkoa wa magharibi baada ya kukagua ujenzi wa ukumbi wa mitihani uliotekelezwa kupitia TASAF ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akitoa maelekezo alipotembelea ukumbi wa mitihani katika skuli ya Fujoni iliyopo mkoa wa magharibi baada ya kukagua ujenzi wa ukumbi wa mitihani uliotekelezwa kupitia TASAF ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akizungumza na walimu katika skuli ya Fujoni iliyopo mkoa wa magharibi baada ya kukagua ujenzi wa ukumbi wa mitihani uliotekelezwa kupitia TASAF ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akikagua soko la samaki Nungwi mkoa wa Kaskazini ambalo limekarabitiwa kupitia mradi wa SWIOFISH. 

(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)

…………………………………………………………………………………………………

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo amefanya ziara ya kikazi ya kukagua miradi inayotekelezwa pande mbili za Muungano visiwani Zanzibar na kuonesha kuridhishwa na utekelezaji wake.

Akiwa ameambatana na Naibu Waziri wake Mhe. Hamad Hassan Chande alikagua miradi mitano katika mikoa mbalimbali ya Unguja Zanzibar ambapo alisema utekelezaji wa miradi hiyo ni matunda ya Muungano ambao sote tunajivunia.

Alisema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejipanga kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo huku akisisitiza kuwa imejipanga kuondoa changamoto 10 za Muungano zilizosalia. 

Aidha, aliwataka wasimamizi wa miradi kusimamia kwa umakini fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Muungano ili zilete matokeo mazuri.

“Binafsi nimefarijika sana kutembelea miradi hii na kukuta inatekelezwa kwa ufanisi lakini niwasihi muhakikishe gharama zinazotumika zinawiana na ubora wa miradi hii. Naagiza Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) msimamie majengo haya kwa ukaribu mkizangatie thamani ya fedha,” alisema.

Hata hivyo Waziri Jafo alielekeza uongozi kukamilisha jengo la huduma ya mama na mtoto lililoanza kujengwa na kuachwa kwa kipindi kirefu bila kumalizika pembeni ya kituo cha afya cha Kianga katika Wilaya ya Magharbi Mkoa wa Mjini Magharibi kujengwa upya kwa kutumia fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na kukamilika kufikia Oktoba mwaka huu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uratibu wa Shughuli za Serikali anayeshughulia Muungano Zanzibar Khalid Bakar Hamran aliwataka wananchi waibue miradi ambayo wana changamoto ili waweze kutatuliwa.

Alisema fedha za TASAF zimeongezeaka kutoka sh. bilioni 12 za awali hadi 21.2 ambazo zitawawezesha kuendelea kutekeleza miradi ya TASAF katika sekta za afya, elimu na maji.

Hamran aliahidi kuwa mradi huo utaendelea kuboresha sekta ya elimu kwa kutatua changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa pamoja na kumbi za kufanyia mitihani katika skuli za sekondari na ofisi za walimu.

Aliahidi kutekeleza agizo la Waziri Jafo la kuchukua hatua ya kukamilisha jengo la mama na mtoto kando ya kituo cha afya cha Kianga ili lianze kuhudumia wananchi. 

Miongoni mwa miradi aliyoitembelea ni pamoja na kituo cha afya cha Kianga, Ukumbi wa kufanyia mitihani katika Shule ya Sekondari Fujoni na vyumba vitatu vya madarasa na jengo la utawala katika Skuli ya Sekondari Mahonda Mkoa wa Magharibi. Miradi hiyo inatekelezwa kupitia fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Miradi mingine aliyotembelea ni soko katika eneo la Kinyasini kupitia mradi wa MIVARF na soko la samaki lililokarabatiwa kupitia fedha za mradi wa SWIOFISH katika eneo la Nungwi mkoa wa Kasakaz

Post a Comment

Previous Post Next Post