WAITARA AMTAKA MKANDARASI KUFANYA KAZI USIKU NA MCHANA KUKAMILISHA UPANUZI WA KIWANJA CHA NDEGE MUSOMA

 

Meneja wa Wakala wa Barabarani Nchini TANROADS Mhandisi  Felix Ngaile, akifafanua jambo, wakati wa Kikao cha Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (hayupo pichani) na Watendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara, kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, akifafanua jambo, wakati wa Kikao chake na  Watendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara, kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara

Sehemu ya Watumishi wa taasisi taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara (hayupo pichani) alipokutana nao  katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Meneja wa Wakala wa Barabarani Nchini TANROADS Mhandisi  Felix Ngaile, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (wa tatu kulia) alipokagua Kiwanja cha Ndege cha Musoma, Mwishoni mwa wiki.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, akitoa Maelekezo kwa Meneja Mradi wa Kampuni ya M/s Beijing Construction Engineering Group Company Limited, Ma li Gong (wa pili kushoto), Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mhandisi Felix Ngaile alipogua kiwanja cha Ndege cha Musoma, Mkoani Mara.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, akiangalia urefu wa Kiwanja cha Ndege cha Musoma, alipokagua kabla ya ujenzi wake kuanza. Ujenzi wake utachukua miezi 20 na utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 35.

Mafundi wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), wakifunga nondo katika Daraja linalounganisha Mtaa wa Mwangaza na Msati, lililoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha, Wilayani Tarime, Mkoani Mara.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (wa pili kulia) akimsikiliza Meneja wa Wakala wa Barabarani Nchini TANROADS Mhandisi  Felix Ngaile, akimweleza hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Daraja linalounganisha Mtaa wa Mwangaza na Msati, lililoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha, Wilayani Tarime, Mkoani Mara.

……………………………………………………………………………………

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, amemtaka mkandarasi wa kampuni ya M/S Beijing Construction Engineering Group Company Limited kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha kwa wakati mradi wa upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Musoma. 

Mradi huo utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 30 unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 20 utahusisha barabara ya kuruka na kutua ndege, barabara ya maegesho ya ndege na jengo la zima moto. 

Akizungumza mara baada ya kukagua kiwanja hicho mkoani Mara, Naibu Waziri Waitara amesema kukamilika kwa kiwanja hicho kutapandisha uchumi wa mkoa na kukuza utalii katika ukanda huo. 

“Mradi huu ni muhimu sana kwa uchumi wa Kanda ya Ziwa kwani kiwanja hiki kitapunguza gharama kubwa wanazotumia wananchi wa mkoa huu kwa kulazimika kutumia kiwanja cha Mwanza na badae kuingia kwenye magari kuja Musoma na Wilaya nyingine za Mkoa” amesema Naibu Waziri Waitara. 

Naibu Waziri Waitara ameutaka Wakala wa Barabarani Nchini (TANROADS) kuhakikisha unasimamia mradi huo ili ukamilike kwa wakati na viwango vinavyokubalika kulingana na mkataba. 

Naye Meneja wa Kiwanja cha ndege cha Musoma Mohammed Makau amesema kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo kutaruhusu ndege aina ATR 42 na Dash 8 Q 400.

Katika Hatua nyingine Naibu Waziri Waitara amekagua maendeleo ya ujenzi wa daraja linalounganisha mtaa wa Mwangaza na Msati, lililopo wilayani Tarime lililokatika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini  na kuridhishwa na ujenzi wake. 

“Nawapongeza sana TANROADS hasa Meneja wa mara maana siku limekatika nilipigiwa sim una mimi nikawasiliana na nyinyi na hapo hapo na nimeelewa kuwa mnafanya kazi usiku na mchan, hongereni sana’ Amesema Naibu Waziri Waitara. 

Naye Meneja wa TANROADS Mara, Mhandisi Felix Ngaile amesema kazi hiyo itakamilka kabla ya jumatatu na  magari yataruhusiwa kuanza kupita ili kuwarahisishia wananchi huduma za usafirishaji kutoka eneo moja kwenda jingine. 

Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo  amezungumza na watumishi wa taasisi zilizo chini ya WIzara hiyo na kuwataka kuongeza bidii kazini kwani Serikali haitavumilia mtumishi atakayeshindwa kutimiza majukumu yake kwa sababu ya uzembe. 

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mwita Waitara amekamilisha ziara yake ya siku mbili mkoani Mara kwa kukagua miundombinu ya uchukuzi. 

  

(Imetolewa na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Post a Comment

Previous Post Next Post