TBS YAENDELEA NA UKAGUZI WA BIDHAA ZA VYAKULA NA VIPODOZI WILAYANI SIKONGE MKOANI TABORA

 

Mkaguzi wa TBS Bw,Sileje Lushibika akimsajili mfanyabiashara, Bw Hamza Rashid mara baada ya kukamilisha ukaguzi katika eneo la Sokoni Wilayani Sikonge-Tabora. Wafanyabiashara wanatakiwa wasajili majengo yao ili wapate kibali kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni za uuzaji, usambazaji na uhifadhi wa bidhaa za chakula na vipodozi 

Mkaguzi wa TBS, Bi Zena Mushi akiendelea na zoezi la usajili kwa wafanyabiashara wa bidhaa ya chakula na vipodozi katika kata ya Tutuo, Wilayani Sikonge- Tabora. Wafanyabiashara hao walifurahia kusogezewa huduma hiyo na kulitaka Shirika lifanye zoezi hilo Nchi zima 

Mkaguzi wa TBS, Bw. Sileja Lushibika akiendelea na ukaguzi wa bidhaa za chakula na vipodozi sambamba na kukagua ukomo wake wa matumizi, pamoja na kusajili majengo ya bidhaa hizo katika kata ya Sikonge wilayani Sikonge-Tabora 

Mkaguzi wa TBS Bw.Sileje Lushibika akiendelea na ukaguzi wa majengo ya bidhaa za chakula na Vipodozi katika eneo la Ipole, wilayani Sikonge ambapo alibani uwepo wa vipodozi vilivyokatazwa ambavyo viliondolewa kwa ajili ya kutekekezwa.

******************************

Shirika la Viwango Tanzania limeendesha program ya kukagua bidhaa ya vyakula na vipodozi Wilayani sikonge mkoani Tabora ili kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa zilizobora.

Zoezi hilo la ukaguzi limelenga pia utoaji wa elimu kwa wafanyabiashara kuhusu alama ya viwango kwenye bidhaa ambazo wananunua na kuuza.

Post a Comment

Previous Post Next Post