JAFO ATOA MIEZI SITA KWA UONGOZI WA MACHINJIO YA KISASA KIZOTA DODOMA KUREKEBISHA CHANGAMOTO ZAO

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akisikiliza maelezo kuhusu utendaji wa machinjio ya kisasa katika eneo la Kizota jiji Dodoma alipofanya ziara ya kikazi kukagua utunzaji wa mazingira machinjioni hapo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akiwa katika ziara ya kukagua utuzanjaji mazingira alipofanya ziara ya kikazi katika kiwanda cha kurejeleza taka za plastiki cha Future Colorful Limited kikichopo Kizota jijini Dodoma. Kushoto ni Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC) Kanda ya Kati Flanklin Rwezimula na mmiliki wa kiwanda hicho Wang Zuo Min.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akisikiliza maelezo kuhusu utendaji wa machinjio ya kisasa kutoka kwa Meneja wa machinjio hayo katika eneo la Kizota jiji Dodoma Chacha Mwita alipofanya ziara ya kikazi kukagua utunzaji wa mazingira machinjioni hapo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akiwa katika ziara ya kukagua utuzanjaji mazingira alipofanya ziara ya kikazi katika kiwanda cha kurejeleza taka za plastiki cha Future Colorful Limited kikichopo Kizota jijini Dodoma.



Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC) Kanda ya Kati Flanklin Rwezimula akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali kwa waandishi wa habari wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo katika kiwanda cha kurejeleza taka za plastiki cha Future Colorful Limited kikichopo Kizota jijini Dodoma.  (PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS).

=========  =======  ======  ======

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo ameupa uongozi wa machinjio ya kisasa ya Kizota jijini Dodoma miezi sita kurekebisha changamoto ya utiririshaji wa majitaka ovyo.

Jafo ametoa agizo hilo leo Aprili 8, 2021 alipofanya ziara ya kikazi katika machinjo hiyo kwa ajili ya kukagua udhibiti wa majitaka na utunzaji wa mazingira kwa ujumla.

Alisema kuwa kila kiwanda lazima kiwe na mpango wa namna ya kuyatibu majitaka na kudhibiti utiririshaji wake kuepusha yasiende kwenye makazi yao watu na kusababisha madhara ya kiafya.

“Nafahamu machinjio hii ni miongoni mwa machinjo kubwa na ina soko kubwa katika nchi za Mashariki ya Kati wananunua nyama nami nimekuja hapa kujiridhisha kuhusu suala zima la utiririshaji wa majitaka,” alisema.

Alimuelekeza Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC) Kanda ya Kati Flanklin Rwezimula kufuatilia kazi ya kuhakikisha machinjio hiyo inatengeneza mfumo wa kutibu majitaka haraka. 

Post a Comment

Previous Post Next Post