WAZIRI NDALICHAKO AWATAKA WATUMISHI WA WIZARA HIYO KUZINGATIA WELEDI NA KUACHA KUTUMIA LUGHA ZA KIBABE

 

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako,akizungumza leo April 8,2021 jijini Dodoma wakati  akizindua mkutano wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo.

 

Baadhi ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako (hayupo pichani)  wakati  akizindua mkutano wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo uliofanyika leo April 8,2021 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo,akizungumza kwenye Mkutano wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo uliofanyika leo April 8,2021 jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe,akizungumza kwenye Mkutano wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo uliofanyika leo April 8,2021 jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Carolyne Nombo,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mkutano wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo uliofanyika leo April 8,2021 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya Ualimu ambaye pia ni Katibu wa Baraza Bw.Huruma Mageni akitoa taarifa wakati wa uzinduzi wa Mkutano wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo uliofanyika leo April 8,2021 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mwl.Deus Seif,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki mara baada ya kuzinduliwa kwa Mkutano wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo uliofanyika leo April 8,2021 jijini Dodoma.

 

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kuzindua Mkutano wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo uliofanyika leo April 8,2021 jijini Dodoma.

…………………………………………………………………………………………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako,amewaonya baadhi ya Watumishi  wa Wizara hiyo wanaotumia ubabe na matumizi ya lugha ambazo si sahihi na kuwasumbua wateja ndani ya wizara hiyo.

Prof Ndalichako ametoa kauli hiyo leo April 8,2021 jijini Dodoma wakati  akizindua mkutano wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo amewataka watumishi wote wa Wizara hiyo kuzingatia weledi na kuacha kutumia lugha za ubabe wanapowahudumia wateja wao

”Bado kuna changamoto ya baadhi ya watumishi wa wizara yangu kutumia lugha za ubabe wakati wakiwahudhumia wateja wao hivyo natoa onyo kwa mtu atakayeonakana tutamchukulia hatua kali za kinidhamu”amesema Prof.Ndalichako

Aidha amesisitiza nidhamu makazini hasa kuwa waungwana na wastaarabu kwa wananchi, haiwezekani mtu amefunga safari amefuata huduma toka asubuhi hadi jioni yupo tu na bado unamwambia arudi kesho.

“Huu siyo uungwana ni kuwagombanisha wananchi na serikali yao, tabia hii sitaki kuiona nachotaka ni utii, ufanisi na utendaji kazi uliotukuka,” Amesema.

Aidha Prof.Ndalichako amaeushtukia mfumo wa usajili wa shule ambao umekua ni kichochoro cha upigaji pesa ambapo zaidi ya shilingi bilioni moja hazijulikani na kumuagiza katibu mkuu kulishulikia suala hilo.

Aidha Prof.Ndalichako ametoa onyo kwa  halmashauri zote hapa nchini ambazo zimekua na tabia ya kufanya udanganyifu kwenye uandikishwaji wa wanafunzi ambao wanamaliza darasa la Saba kwa kuwaondoa kwa kuwa hawana uwezo wa kufaulu.

Prof.Ndalichako amesema kuwa amebaini kuwa kuna  halmashauri ambazo zimekuwa zikiondoa majina ya wanafunzi wanaotakiwa kufanya mitihani ya darasa la saba kwa kuepuka kwamba watafeli na kuziletea sifa mbaya halmashauri hizo.

Ametoa onyo kwa maafisa elimu wa halmashauri hizo na walimu wakuu kwenye shule ambazo zimeondoa majina ya wanafunzi hao kuacha mara moja na wale watakaokaidi hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

” Nimepata taarifa kutoka kwa raia mwema kuhusu hii tabia kwenye Halmashauri nchini ambapo kwa makusudi kabisa maafisa elimu na walimu wakuu wanaondoa majina ya wanafunzi wenye uwezo mdogo kwa kuepuka kwamba watafeli na halmashauri zao kuonekana zinafanya vibaya, wanachokifanya wanawarudisha hao wanafunzi darasa la sita” amesema Prof. Ndalichako.

Amesema serikali imeamua kuwekeza kwenye elimu kwa kutoa elimu bila malipo hivyo kitendo cha kuwaondoa wanafunzi hao ni kuchongesha serikali na wananchi kwani hao wanafunzi wanaorudishwa nyuma bila mpango wa serikali wanakua hawapo kwenye hesabu ya elimu bila malipo.

” Unajua serikali tunatenga fedha nyingi kwenye Sera hii ya elimu bila malipo, hawa maafisa elimu na walimu wakuu wanavyowarudisha nyuma hawa wanafunzi wakati serikali ishatenga bajeti yao inaajua wanamaliza matokeo yake mwaka unaofuata idadi ya wanafunzi inaongezeka nje ya kiasi kilichopangwa,” Amesema Prof Ndalichako.

Waziri Ndalichako amewatoa hofu pia watumishi wote wenye sifa za kupandishwa madaraja kuwa watapandishwa kwani tayari Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk Leonard Akwilapo ameshapeleka taarifa zao Ofisi ya Rais Utumishi.

” Niwaombe mfanye kazi kwa bidii ili kuipa sifa zaidi wizara yetu, Rais Mama Samia ameendelea kutuamini ndio maana mnaona timu yote Mimi, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wote tumerudishwa hajatubadilisha,maana yake anatuamini sana, twendeni tukafanye kazi kwa weledi kwa kufuata taratibu na sheria zetu na watakaofanya vizuri basi tunawapandisha madaraja maana inakua ni haki yao, mtu akifanya vizuri lazima apewe haki yake” amesema.

Post a Comment

Previous Post Next Post