Wizara ya Maji imewaahidi kuwaunga mkono wawekezaji wa viwanda nchini na kuwataka kutengeneza mabomba yenye ubora na bei halisi.
Hata hivyo Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameagiza mradi wa maji wa Mbwita uliopo Tandahimba kuhakikisha unakamilika haraka baada ya kusuasua kaa muda mrefu.
Akiwa katika ziara yake ya siku mbili ya kutembelea viwanda vinavyozalisha miundombinu ya maji yakiwemo mabomba makubwa, Aweso amemtaka Mkurugenzi wa Wakala wa Usambazaji Maji Vijijini (RUWASA) Mhandisi Clemence Kivegalo kuhakikisha ndani ya wiki moja maboma waliyoyatelekeza katika kiwanda cha Pipe yaondoke haraka
Amesema, kumekuaa na malalamiko mengi sana kuhusiana na kusuasa kwa miradi a kutoa kisingizio viwanda vinachelewesha mabomba wakati mambomba yapo tayari na wameshindwa kuyafuata.
"Sasa hivi tunataka kazi ifanyike nakuagiza Mkurugenzi wa RUWASA uhakikishe mabomba haya yanaondoka kiwandani, mnalalamika mabomba hayafiki kumbe wenyewe mnachelewesha miradi ambayo wananchi wanahitajika wapate maji," amesema
Aweso, ameshangaa kuona mradi uliokuwa unatakiwa uchukue mwaka mmoja unachukua zaidi ya miaka miwili kitu ambacho sio sahihi na wanawakosea wananchi.
Aidha, amezitaka mamlaka zote kuacha kuwa wadanganyifu baada ya kutembelea viwanda vinne amegundua kuwa wanafanya uzalishaji mkubwa sana wa mambomba ya aina zote na yaliyokidhi viwango vyote.
Akizungumzia suala la rasilimali fedha baada ya kusikiliza changamoto kutoka kwa Viwanda, Waziri kwa njia ya simu amemuaguza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji kuhakikisha malipo yanafanyika kwa wakati ili miundo mbinu iweze kwenda kwenye miradi na kuendelea na ujenzi.
Amesema, kuna miradi inachukua muda mrefu kutokana na kusuasua kwa malipo na kupelekea kiwanda kusitisha uzalishaji wa mabomba hayo na amewataka inapotokea changamoto kama hiyo wasisite kusema kwani serikali inawapatia Wizara ya Maji fedha kila mwezi kwa ajili ya miradi ya maji.
"sitaki kuona miradi ya maji inakuwa chechefu, nimeona viwanda vinafanya uzalishaji mkubwa sana ila Serikali inatoa fedha katika Wizara ya Maji kila mwezi sasa naagiza madeni yote yalipwe ili miundombinu iendw miradi iendelee kujengwa nataka kwenye wiki ya maji nizindue miradi mipya na wananchi wanywe maji safi na salama,"
Kabla ya kuanza kwa ziara hiyo,Waziri wa Maji Aweso amemtembela Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Abubakar Kunenge ambapo miongoni mwa ajenda walizokubaliana ni kuendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa maji Safi na uhakika Dar es salaam ili kukidhi haha za wananchi.
Aidha Waziri Aweso amemshukuru na Kumpongeza RC Kunenge kwa namna anavyosimamia miradi ya Maji na kuhakikisha inakamilika kwa wakati.
RC Kunenge amemshukuru Waziri Aweso kwa kumtembelea na pia amesema kwa utendaji kazi wanaoonyesha Wizara ya Maji na DAWASA anaamini tatizo la uhaba wa Maji Dar es salaam litabaki kuwa historia.
Pamoja na hayo ametoa pongezi kuwa wamilimiki wa viwanda kwa kuunda mkono juhudi za Rais Dkt John Pombe Magufuli za Tanzania ya Viwanda na hilo limewezekana kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanyika nchini kupitia sekta ya Viwanda.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akipata maelezo mbalimbali kutoka kwa wataalamu wa Kiwanda cha Pipe kinachojishughulisha na utengenezaji wa Miundo mbinu ya maji mabomba makubwa na madogo kilichopo Jijini Dar es Salaam. Waziri Aweso amefanya ziara ya siku mbili katika Viwanda hivyo na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuwataka wakandarasi kutumia rasilimali za ndani kwani zina ubora ule ule na zinapunguza muda wa kuagiza kutoka nje ya nchiAina mbalimbali za mabomba yanayotengenezwa katika Viwanda vilivyopo Tanzania.