MBUNGE JERRY SLAA AMSHUKURU JPM, JIMBO LA UKONGA KUPATA MAJI

 



Meneja wa Mkoa wa Kihuduma DAWASA Ukonga Mhandisi Damson Mponjoli akitoa maelezo mbalimbali ya mradi wa Maji wa Pugu Kisarawe sambamba na kutembelea tanki la maji kwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga Jerry Slaa  alipotembelea maeneo yatakayonufaika na mradi huo ulioanza kutoa huduma kwa wakazi wa Jimbo lake.
Meneja wa Mkoa wa Kihuduma DAWASA Ukonga Mhandisi Damson Mponjoli akionesha ramani itakayonufaika  mradi wa Maji wa Pugu Kisarawe sambamba na kutembelea tanki la maji kwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga Jerry Slaa  alipotembelea maeneo yatakayonufaika na mradi huo ulioanza kutoa huduma kwa wakazi wa Jimbo lake.

Na Zainab Nyamka,Michuzi Tv

MBUNGE wa Jimbo la Ukonga Jerry Slaa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kutimiza adhma yakila mtanzania kupata maji safi na salama baada ya mradi wa maji Pugu - Kisarawe kukamilika.

Aidha, Slaa ameweka wazi kuridhishwa na utendaji kazi wa Meneja wa Mkoa wa Kihuduma DAWASA Ukonga Mhandisi Damson Mponjori katika utekelezaji wa miradi ya maji kwa asilimia 100.

Ameyasema hayo baada ya kutembelea ofisi ya Dawasa Ukonga na kupata taarifa mbalimbali za miradi inayoendelea kutekelezwa ndani ya Jimbo lake.

Slaa amesema, Meneja wa Ukonga anafanya kazi kubwa sana na ameridhishwa na utendaji kazi  wake  na anaamini katika muda mfupi huduma ya maji safi na salama yatapatikana kwa wananchi wake wote.

"Unajua mimi nimekulia huku Ukonga nalifahamu vizuri jimbo langu na tabu ya maji waliyokuwa wanapata, tulikua tunatumia maji ya visima tukaanza kununua ya madumu ila kwa sasa wananchi wananchi wanatumia maji kutoka Dawasa," amesema.

Slaa  amesema, mradi wa maji Kisarawe umeleta matumaini mapya  kwa wananchi wa Ukonga na amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwa na maono makubwa ya kutoa maji Ruvu Juu kupitia Kibamba hadi Kisarawe na kuyaleta Ukonga.

"Nimshukuru Rais wang Dkt John Pombe Magufuli, ametufanya Ukonga tupate maji kwani baada ya mradi kufika Kisarawe kutokea Kibamba imekuwa ni neema kwetu  sisi wana Ukonga, na sasa maji tumeanza kuyaona," amesema Slaa.

Kwa upande wa Meneja wa Dawasa Mkoa wa Kihuduma Ukonga Mhandisi Damson Mponjori amesema mkoa wa Kihuduma Ukonga una jumla ya kata 9 zinazohudumiwa na DAWASA.

Amesema kwa sasa sehemu kubwa  wananchi waliokuwa  hawapati huduma ya maji, wameanza kupata huduma hiyo kupitia mtandao wa zamani wa Gopu na miundo mbinu mipya inayoanza kulazwa katika maeneo tofauti.

"Wananchi wameanza kupata maji kupitia mtandao wa zamani, lakini pia tunaendelea na urekebishaji wa miundombinu ya zamani iliyokuwa inasababisha upotevu wa mkubwa wa maji.

Mponjori amesema, DAWASA inaendelea na ulazaji wa mabomba makubwa na madogo ili kuyafikisha maji karibu zaidi kwa wananchi katika kata Pugu

 Pugu stesheni ,Majohe,G/mboto, Kipunguni ,Buyuni na Ukonga.

Aidha, ameeleza kuwa Mtaa wa Pugu Kinyamwezi tayari wameshalaza mtandao wa mita 1000 , Pugu Dampo mita 600, Pugu Kajiungeni mita 300 Kigogo Fresh mita 300,  Pugu Kajiungeni na Pugu Dampo ambapo wameanza kupata Huduma ya maji na  zoezi hilo ni endelevu.

Post a Comment

Previous Post Next Post