WAZIRI WA UJENZI,UCHUKUZI NA MAWASILIANO AKAGUA UBORESHAJI BANDARI DAR, ATOA MAAGIZO

 Na Said Mwishehe, Michuzi TV.

 
WAZIRI wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Dkt.Leonard Chamuriho, amefanya ziara katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzani(TPA), pamoja na kukagua shughuli mbalimbali za miradi ya kuendeleza Bandari ya Dar es Salaam ambapoa emetumia nafasi hiyo kutoa maagizo kadhaa yakiwemo ya miradi yote inayoendelea kujengwa kukamilika kwa wakati.

Akizungumza baada ya kutembelea TPA na kuona shughuli za ujenzi wa miradi ya kimkakati ya uboreshaji wa bandari ya Dar es Salaam, Dkt.Chamuriho amesema amerdhishwa na kasi ya maboresha yanayoendelea bandari ya Dar es Salaam lakini ametoa maagizo miradi yote ya kuboresha bandari inapaswa kukabidhiwa kwa wakati na si vinginevyo.

"Nimeona na kukagua shughuli mbalimbali ambazo zinaendelea hapa bandari ya Dar es Salaam , kasi ya ujenzi inaendelea vizuri, kila hatua ya ujenzi ambayo itakamilika tutaendelea kupokea lakini mwisho kasi baada ya kukamilika kwa eneo lote la mradi basi Rais wetu mpendwa Dkt.John Magufuli ambaye aliweka jiwe la msingi, ndio atakuja kuzindua rasmi.

"Nafahamu pamoja na maboresho mbalimbali yanayoendelea pia kuna jumla ya magati nane yanaboreshwa katika bandari hi ya Dar es Salaam na kwamba kati ya hayo manne yamekamilika na yameanza kutumika likiwemo hili gati namba tano ambalo leo tumekabidhiwa na mkandarasi linataanza kufanya kazi ya kutoa huduma."Amesema Dkt.Chamuriho.

Amewapongeza TPA kwa kufanikisha usimamizi huu japokuwa changamoto ni kwamba mradi huo."Maagizo yangu TPA endeleeni kusimamia kuhakikisha hii miradi yote inakamika kwa wakati au kabla ya ule muda uliokuwa umepangwa.

"Nisisitize hapa hapa najua kuna miradi ambayo ujenzi wake inaonesha ujenzi utafanyika ndani ya miezi 36 lakini namuamini mkandarasi na uwezo wake mkubwa alionao, hivyo wafanye ndani ya miezi 18 na hayo ni maelekezo yangu kwenu.”

Kuhusu ziara yake, amesema ameamua kufanya ziara hiyo kwa ajili ya kuangalia mradi huo wa kimkakati wa kuboresha bandari ya Dar es Salaam,na kwamba mradi huo wa awamu ya kwanza unalenga kuboresha magati nane likiwemo geti namba 0, gati namba moja, mbili, tatu na namba nne yaendelea kutoa huduma baada ya kukamilika, na kutokana na kukamilika kwa magati hayo meli kubwa sasa zinaingia kuleta magari.

Amesema katika gati ambalo linatumika kushusha magari, huduma zimeboreshwa kwani kwa sasa magari 80 hadi magari 100 yanateremshwa kwa saa kutoka magari 40 kabla ya maboresho hayo huku akifafanua maboresho hayo yanafanywa kwa mkopo wa fedha za Benki ya Dunia pamoja na fedha zinazotolewa na Serikali ya Tanzania, madi huo ni mkubwa.

Amesema katika maboresho hayo wameongeza kina cha bahari na hivyo meli kubwa zinaingia kwa urahisi, hivyo kazi iliyobakia ni kuanza kwa kazi ya kuchimba njia ambayo meli kubwa itatumika kupitia, na mradi huo uliokuwa miezi 36 lakini sasa wamekubaliana utekelezwe ndani ya miezi 18 ili meli kubwa zianze kuingia kwa urahisi.

Akifafanua zaidi kuhusu ziara yake, amesema amekuagua eneo ambalo litakuwa linapokea reli tatu ndani ya Bandari ya Dar es Salaam ambako kutakuwa na njia saba, ambapo ametoa maelekezo TPA wakikishe kwenye ukarabati huo wa njia za reli, reli ya TAZARA isiharibiwe kwani ndio inayotumika kwenye kuleta vifaa ambavyo vinatumika katika ujenzi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere.

Dkt.Chamuriho pia amesema anafahamu kuwa bado kuna bandari kavu zinatoa huduma lakini maelekezo yake kwa TPA ni kuhakikisha bandari kavu ya Kwala inaanza kutumika na makasha yote(kontena)ziwe zianze kuhifadhiwa huko na wadau wote 32 ambao wako bandari ya Dar es Salaam wawepo kwa Kwala pamoja na mifumo yote ya utoaji huduma iwepo Kwala.

"Kuhusu mifumo ya utoaji huduma inayorahisisha katika kutoa huduma pamoja na eneo la rasilimali watu nitakuja siku nyingine kuikagua, maana siwezi kutoa maelekezo wala maagizo yoyote kwenye maeneo hayo mawili kwani, sijafanya ukaguzi wowote,"amesema Dkt.Chamuhiro.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko ametumia nafasi hiyo kutoa maelezo kuhusu hatua mbalimbali za uboresha wa bandari ya Dar es Salaam zinavyoendelea na hatua ambazo zimefikia.

"Malengo yaliyopo mpaka kufikia mwaka 2025 ambao ndio mwisho wa miradi iwe imekamilika na tunataka tuwe tunapokea tani milioni 25 kwa mwaka kutoka za sasa ambazo tani 17.5 ,Juni mwaka 2020.Tumejipanga na tutahakikisha miradi hiyo inakamilia kwa wakati kama ambavyo Serikali imeagiza."

Amesisitiza miradi hiyo kila inapokamilika wataendelea kuipokea na kuanza kuitumia wakati wakisubiri uzinduzi wake."Katika maboresho haya ya bandari pia tunataka kuwa na uhakika wa meli kubwa kuingia kwenye bandari yetu hii, katika miradi hii ya maboresho tunayo mikataba mitatu kwa ajili ya kuboresha maeneo mbalimbali na ndani yake kuna mikataba mingine."

Amesisitiza maboresho hayo ya miundombinu kwenye bandari ya Dar es Salaam yanakwenda kuongeza kasi ya utoaji wa huduma na kwenye eneo la utoaji huduma kua mfumo ambao umeanza kutumika katika kuondoa kontena pamoja na mafuta na mfumo huo umetengenezwa na watalaam wa TPA."Kubwa zaidi kwenye mapinduzi haya ni ule mradi wa kutoa huduma za pamoja , tunao wadai wa taasisi za umma 34 ambazo zinafanya kazi bandarini lakini tunazo taasisi binafsi, kwa hiyo hao wote wanamhudumia mteja moja.

"Sasa anapita maeneo mengi kutafuta vibali, lakini mfumo wa TPA unakwenda kuhudumia kwa pamoja, mteja atakaa nyumani ataingia maombi yake na kupata majibu kutoka kwa watu wote hao wanaomhudumia.Mfumo huo wa huduma za pamoja ni muhimu sana."Amesema Mhandisi Kakoko.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dk.Leonard Chamuriho (aliyeinama kulia) akiweka kamba kwenye nanga baada ya meli kubwa ya mizigo ya African Finch kuwasili katika Bandari ya Dar es Salaam.Kutia nanga kwa meli hiyo ni ishara ya kukamilika kwa gati namba tano ambalo tayari limeanza kutumika kutoa huduma. Wengine ni maofisa wa TPA wakisaidia kuvuta na kuweka kamba katika gati hilo.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dk.Leonard Chamuriho(katikati) akizungumza wakati wa tukio la kukabidhiwa gati namba tano katika Bandari ya Dar es Salaam.Gati hilo ni sehemu ya maboresho katika bandari hiyo.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mhandisi Deudedit Kakoko.
Meli kubwa ya mizigo ya African Finch ikiwa imewasili kwenye gati namba tano katika Bandari ya Dar es Salaam.Gati hilo limeboreshwa ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha bandari hiyo.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dk.Leonard Chamuriho (katikati) akipata maelezo kutoka kwa moja ya maofisa wa Bandari ya Dar es Salaam baada ya Waziri huyo kufanya ziara ya kukagua maboresho ya miundombinu kwenye bandari hiyo.Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mhandisi Deusdedit Kakoko.
Mmoja ya wasimamizi wa maboresho ya miundombinu katika Bandari ya Dar es Salaam (wa pili kulia) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dk.Leonard Chamuriho (hayupo pichani) baada ya kufanya ziara katika bandari hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko akiaangalia taarifa ya shughuli za bandari ya Dar es Salaam kabla ya kuwasili kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dk.Leonard Chamuriho ambaye alifanya ziara kwenye bandari hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mhandisi Deusdedit Kakoko (kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dk.Leonard Chamuriho baada ya kufanya ziara katika bandari ya Dar es Salaam.
Mmoja ya watalaamu katika Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) akitoa ufafanuzi kuhusu maboresho yanayoendelea katika Bandari ya Dar es Salaam baada ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dk.Leonard Chamuriho alipofanya ziara ya kutembelea bandari hiyo.
Shughuli za upakuaji mizigo katika moja ya meli zikiendelea katika Bandari ya Dar es Salaam.
Nondo zikiwa zimesukwa kabla ya kumwaga zege ikiwa ni sehemu ya uboreshaji wa gati zilizopo katika Bandari ya Dar es Salaam.

Post a Comment

Previous Post Next Post