IKIWA Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Wanawake Duniani, wanawake kutoka Tume ya Madini Makao Makuu wametembelea gereza la wanawake lililopo jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Wanawake Duniani.
Akizungumza kabla ya kuanza kwa ziara hiyo, Afisa Utawala wa Tume ya Madini, Joyce Rweyemamu amesema ni sehemu ya kugusa jamii hususan wanawake walioko magerezani ambao wamesahaulika.
"Wanawake wengi wamekuwa wakigusa jamii kwa namna mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwasaidia yatima,wajane na wagonjwa lakini sisi kama wanawake kutoka Tume ya Madini tumeamua kufanya kitu cha tofauti kwa kuwatembelea wanawake waliopo magerezani kama sehemu ya kuwatia moyo na kufahamu kuwa wanatengenezwa na kuwa bora mara baada ya kumaliza kutumikia adhabu ya kifungo." Amesema Rweyemamu.
Katika hatua nyingine, Rweyemamu amewataka wanawake katika Taasisi nyingine na jamii kwa ujumla kuwa na moyo wa kugusa jamii kwa kuwasaidia watu wenye uhitaji.