WANAFUNZI WA PASIANSI WATEMBELEA OFISI ZA TTB KANDA YA ZIWA

 Wanafunzi wa Chuo cha Wanyamapori cha Pasiasi leo wametembelea ofisi za Bodi ya Utalii (TTB) kanda ya ziwa zilizopo mkoani mwanza kwa lengo la kupata uwelewa kuhusu majukumu ya TTB na namna inavyoyatekeleza.


Afisa Utalii Mwandamizi, Bi. Glory Munhambo amewaeleza wanafunzi hao kuwa jukumu kubwa la TTB ni kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania ndani na nje ya nchi pamoja na kuishauri serikali katika shughuli zote zinazohusiana na utangazaji wa utalii wa Tanzania.

Bi. Munhambo liwaeleza wanafunzi kuwa “tunatoa taarifa za utalii kupitia maonesho mbalimbali ya utalii yanayofanyika ndani na nje ya nchi, mikutano ya kimataifa, makongamano, matamasha, kuwasilisha mada za utalii katika hafla tunazopata fursa za kushiriki pamoja na kutoa vipeperushi vyenye taarifa za utalii wa Tanzania.

Aliongeza kuwa, kwa kipindi hiki cha mlipuko wa ungonjwa wa COVID 19, Bodi imejikita zaidi kutangaza kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii ya Facebook, Instagram, Twitter na Youtube kwani dunia ya sasa watalii wengi wanatumia mitando ya kijamii kupata taarifa.

Bi. Munhambo alitoa wito kwa wanafunzi hao kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania. 
 
Afisa Utalii Mwandamizi, Gloria Munhambo akiwa na Wanafunzi nje ya ofisi za Bodi ya Utalii Mkoani Mwanza

Post a Comment

Previous Post Next Post