TMDA YAKAMATA MLANGUZI WA DAWA ZA SERIKALI NEWALA

 

TMDA Kanda ya Kusini baada ya kuwekeza katika taarifa za kiintelijensia ilifanikiwa leo 31/01/2021 kutega mtego Wilaya ya Newala Mji na kumnasa Ndg Jamaly Sadick akiuza Dawa za Serikali za Mpango wa Uzazi.

Dawa hizo ni Medroxy Progesterone (vichupa 60) na Microgynon pills (vidonge 3360) zote zikiwa na thamani ya Tshs 300,000/-

Mtuhumiwa na mtoto wake wamefunguliwa jalada polisi RB No.NL/RB/94/221 na yuko ndani kwa hatua zaidi kisheria.

Taarifa hiyo imetolewa na Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma,wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),Gaudensia Simwanza

Post a Comment

Previous Post Next Post