BRELA YATOA UFAFANUZI JUU YA MADAI YA KUKIMBIZA WAWEKEZAJI

 


Wakala  wa  Usajili  wa  Biashara  na  Leseni  (BRELA)  inapenda  kutoa  ufafanuzi  kuhusu  taarifa iliyosambaa  katika  Mitandao  ya  kijamii  juu  ya  BRELA kukimbiza  wawekezaji  kutokana  na changamoto za Mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao (ORS).

Wakala inatambua  dhamana  iliyopewa  na  serikali ikiwa  ni  pamoja  nakuhakikisha  shughuli  za Uwekezaji zinaongezeka nchini, hivyoinaendelea kufanyia kazi changamoto mbalimbali ambazo zimekua  zikionekana kuwanikikwazo  katika  urasimishaji  wa  biashara  kupitia  Mfumo  wa  usajili kwa njia ya mtandao.Ifahamike  kwamba,  mwezi  Mei  2020,  BRELA  kwa  kushirikiana  na  wataalam  wa  mifumo  toka Taasisi  mbalimbaliza  serikali  ilianza  rasmi  kubadilisha  na  kuboresha  mfumo  (System  Re-designing) kwa kuzingatia changamoto zilizopo katika mfumo unaotumika hivi sasa. 

Mfumo huo kwa sasa upo katika hatua za majaribiona utakapo kuwa tayari utakabidhiwa kwa ajili yakuanzakutumikarasmihuku ukisimamiwa   na   wataalam   wazawa   tofauti   na   mfumo   wa   sasa unaosimamiwa na Mzabuni kutoka nje ya nchi.Kukamilika kwa Mfumo huo kutaweza kutatua changamoto zilizopo ikiwa ni pamoja na Maombi kupokelewa  na  kufanyiwa  kazi  na  Ofisa  mmoja,  Ombi  kufanyiwa  kazi  kwa  kuzingatia  ombi lililofika awali (firstcome,first served), kuendelea kuunganisha Mfumo wa BRELA na mifumo ya taasisi  nyingine  kama  Mamlaka  ya  Vitambulisho  vya  Taifa  (NIDA), Mamlaka  ya  Mapato Tanzania(TRA),Kituo  cha  Uwekezaji  Tanzania(TIC), Mamlaka  ya  Mawasiliano  Tanzania(TCRA),  Benki,  Uhamiaji  na Mamlaka  za  utoaji  Leseni  katika  Halmashauri.  

Lengo  kuu  ni kutengeneza mazingira rafiki na wezeshi sio tu kwa wawekezaji bali wafanyabiashara wote.Aidha, katika kuhakikisha kwamba katika kipindi hiki Wadau wa BRELA wanapata huduma nzuri, Wakala  imeanzishaKituo  cha  Miito  na  Huduma  kwa  wateja.  Kituo  hiki  kazi  yake  kuu  ni  kutoa usaidizi wa haraka kwa Wateja wetu wanapokwama wakati wa urasimishaji wa Biashara zao. 

Ni  vyemaumma  ufahamu  kwamba,  muda  wa  usajili  wa  Jinala  biashara  ni  siku  moja(1)na  si zaidi  yasiku  tatu(3)za  kazi,  Usajili  wa  kampuni  ni  siku  tatu(3)na  si  zaidi  ya  siku  tano(5)za kazi, Usajili wa Alama za Biasharana huduma ni kipindi cha siku tisini (90) (kutokana na takwa la kisheria), maombi ya kupataHataza ni siku mia moja na ishirini (120)(kutokana na takwa la kisheria),kupata Leseni ya Kiwanda au Leseni ya Biashara kundi A ni siku moja(1)na si zaidi ya siku tatu(3)za kazi.JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA VIWANDA NA BIASHARAWAKALA WA USAJILI WA BIASHARA NA LESENI

Baada ya kipindi hicho kupita kama usajili haujakamilika Mtejaawasiliane na kituo cha huduma kwa Wateja kupitia namba +255 (0) 222 212 800 au kwa barua pepe maoni@brela.go.tzkwa ajili ya  usaidizi  wa  haraka.

Hivyo  basi,Wakala  inawataka  wadau  wake  kufuata  taratibu  za  usajili ikiwa  ni  pamoja  na  ujazaji  wa  taarifa  kwa  makini  na  uwekaji  wa  viambatanisho  sahihi  ili kuepusha kuchelewa kwa kukamilika kwa usajili.BRELA wakati wote tunapokea maoni ya wadau kwa lengo la kuboresha sio tu mifumo bali pia uendeshaji wa Taasisi yetu“Tunaipa utu wa kisheria biashara yako”

Imetolewa na:

KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO

WAKALA WA USAJILI WA BIASHARA NA LESENI

Post a Comment

Previous Post Next Post