TAARIFA KWA UMMA
MATENGENEZO KWENYE PAMPU ZA KUSUKUMA MAJI MTAMBO WA MAJI RUVU JUU
6/12/2020
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar-es-salaam (DAWASA), inawatangazia wateja wake wa Jiji la Dar es salaam, miji ya Kibaha na Mlandizi mkoani Pwani wanaohudumiwa na mtambo wa maji wa Ruvu Juu, kuwa pamekuwa na upungufu wa maji kufuatia hitilafu katika pampu za kusukuma maji.
Hadi sasa, kazi ya marekebisho ya pampu inaendela vizuri ambapo pampu mbili tayari zinafanya kazi na nyingine moja ipo katika hatua za mwisho za ukamilishwaji.
Kufuatia matengenezo hayo uzalishaji wa Maji umepungua kwa asilimia 20 hali inayopelekea huduma kwenye maeneo mengi hasa yaliyopo Dar es salaam kukosa huduma.
Maeneo yanayoathirika ni pamoja na:
Mlandizi Mjini, Ruvu Darajani, Vikuruti, Disunyara, Kilangalanga, Janga, Mbagala, Visiga, Maili 35, Zogowale, Misugusugu, Tanita, Kibondeni, Kwa Mathias, Nyumbu, Msangani, Kwa Mbonde, Picha Ya Ndege, Sofu, Lulanzi, Gogoni, Kibamba, Kibamba Njia Panda Shule Kibwegere, Mloganzira, Kwembe, Kibamba Hospitali, Kwa Mkinga, Luguruni, Mbezi, Kimara, Ubungo, Makongo, Tabata, Bonyokwa, Kinyerezi, Kisukuru, Kipawa na Kiwalani.
Huduma inatarajiwa katika msukumo (pressure) mzuri kati ya masaa 24 na 36 yajayo.
DAWASA inawaomba radhi wananchi wa maeneo husika kwa usumbufu utakaojitokeza. Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (BURE) au *152*00# na 0735202121 (WhatsApp tu).
IMETOLEWA NA:
OFISI YA MAWASILIANO-DAWASA