Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya,akizungumza wakati wa warsha na uzinduzi wa Chapisho la ”Uendelezaji wa kilimo cha Umwangiliaji na Kukifanya kuwa chenye faida kwa wakulima wadogo Kusini Mwa Bara la Afrika” hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya,akisisitiza jambo wakati wa warsha na uzinduzi wa Chapisho la ”Uendelezaji wa kilimo cha Umwangiliaji na Kukifanya kuwa chenye faida kwa wakulima wadogo Kusini Mwa Bara la Afrika” hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya,(hayupo pichani) wakati wa warsha na uzinduzi wa Chapisho la ”Uendelezaji wa kilimo cha Umwangiliaji na Kukifanya kuwa chenye faida kwa wakulima wadogo Kusini Mwa Bara la Afrika” hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma.
Dkt. Oswald Mashindano kutoka ESRF,akitoa taarifa wakati wa warsha na uzinduzi wa Chapisho la ”Uendelezaji wa kilimo cha Umwangiliaji na Kukifanya kuwa chenye faida kwa wakulima wadogo Kusini Mwa Bara la Afrika” hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya,akizindua rasmi Chapisho la ”Uendelezaji wa kilimo cha Umwangiliaji na Kukifanya kuwa chenye faida kwa wakulima wadogo Kusini Mwa Bara la Afrika” hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya,akionyesha kitabu mara baada ya kuzindua Chapisho la ”Uendelezaji wa kilimo cha Umwangiliaji na Kukifanya kuwa chenye faida kwa wakulima wadogo Kusini Mwa Bara la Afrika” hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha mara baada ya kuzindua Chapisho la ”Uendelezaji wa kilimo cha Umwangiliaji na Kukifanya kuwa chenye faida kwa wakulima wadogo Kusini Mwa Bara la Afrika” hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma.
……………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya amezindua andiko maalum lenye kuonyesha matokeo ya utafiti kuhusu “Uendelezaji wa Kilimo cha Umwagiliaji ili kukifanya kiwe chenye faida kwa Wakulima wadogo Kusini mwa Bara la Afrika Jijini Dodoma.
Akizungumza katika warsha ambayo imeenda sambamba na uzinduzi huo Kusaya amesema kuwa ni muda sasa wa kujikita katika kilimo cha umwagiliaji ili kuwa na uhakika wa kuvuna mazao kwa mwaka mzima.
Kusaya amesema kuwa Lengo kuu la andiko hilo ni kuimarisha uwezo wa kujikimu kwa Wakulima wadogo na kuongeza kuwa ushiriki wao katika kusimamia skeli ndogo za umwagiliaji hususan katika nchi zilizo katika Ukanda wa Jumuia ya Maendeleo Kusini wa Afrika (SADC).
Aidha amesema kuwa andiko hilo lina mkusanyiko wa machapisho mengi ambayo yanatoa mapendekezo mbalimbali ya kisera yatokanayo na tafiti hizo hususan sababu za ufanisi hafifu wa skimu za umwagiliaji maji mashambaji, kuwajengea uwezo Wakulima wadogo katika kuibua na kutekeleza Miradi ya umwagiliaji, uwekezaji katika miundombinu husika na namna bora ya kuendesha kilimo cha umwagiliaji chenye tija zaidi kwa Wakulima wadogo Kusini mwa Afrika.
“Ni dhahiri kuwa utekelezaji wa mradi huu umekuwa muafaka kwa wakati huu nchini kwetu na kwa sekta ya kilimo kwa ujumla kwa kuzingatia umuhimu wa matokeo ya tafiti hizi katika kusaidia juhudi za Serikali kuimarisha usalama wa chakula na lishe pamoja na kukuza kipato kwa Mkulima mmoja mmoja na taifa kwa ujumla halikadharika kuongeza ajira kwa makundi mbalimbali hasa vijana”. amesema Kusaya
Kusaya ameongeza kuwa Mhe. Rais Magufuli wakati akifungua Bunge la 12; Alizungumzia adhima ya Serikali katika kuongeza tija na kukifanya kilimo kuwa cha kibiashara kwa kuahidi kuongeza eneo la umwagiliaji kutoka hekta 561,383 zilizopo sasa hadi kufikia hekta milioni 1.2 mwaka 2025 na lengo kubwa likiwa ni kupunguza utegemezi wa mvua, kujihakikishia usalama wa chakula na lishe, kuongeza upatikanaji wa malighafi za viwandani na pia kupata ziada ya kuuza nje.
Kusaya amekishukuru Chuo cha ardhi na washirika wake ambao ni Taasisi ya utafiti katika Nyanja za uchumi na jamii nchini (ESRF) kwa kutekeleza usambazaji wa matokeo ya mradi kupitia warsha mbalimbali.
“Ninatambua mchango mkubwa wa Taasisi na Mashirika mbalimbali ya Kimataifa katika kutekeleza malengo ya Mradi huu yakiwemo; FANRPAN kutoka Afrika Kusini, Chuo Kikuu cha Taifa cha Australia na Taasisi za umwagiliaji nchini Msumbiji na Zimbabwe kwa kusaidia kukamilika kwa andiko hili”. amesisitiza Kusaya.
Kwa upande wake Dkt. Oswald Mashindano kutoka ESRF amesema kuwa asilimia 80 ya kilimo nchini kinategemea mvua na hivyo kuhatarisha usalama wa chakula jambo ambalo linapaswa kufanyiwa kazi.
Nao baadhi ya wakulima waliozungumza katika warsha hiyo wameiomba serikali kuwasaidia kuondoa kero walizonazo ikiwemo upatikanaji wa masoko,mbegu bora na pembejeo za kilimo