Katibu mkuu wa wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza katika hafla fupi ya kuzindua Maabara wilaya Arumeru mkoani Arusha.
Katibu mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Profesa Ole Gabriel wa Tatu Kushoto akiwa na Balozi wa Poland nchini Tanzania Mara baada ya kuzindua Maabara hizo.
………………………………………………………………………….
Na.Mwandishi wetu Arusha.
Katibu mkuu wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Profesa Elisante Ole Gabriel amezindua maabara mbili ya Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA),Tengeru katika wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
Akizungumza katika hafla fupi ya Uzunduzi wa maabara hizo Profesa Ole Gabriel alisema kuwa sekta ya Mifugo inathamani kubwa katika kuhakikisha kuwa inachangia Pato la Taifa kwa kiwango kikubwa,lakini bado haijafanya hivyo.
Ole Gabriel alisema kuwa vifaa hivyo ni muhimu kwa kuwa itawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo hali ambayo itaongeza uwezo katika masomo yao.
Aidha alisema kuwa Sayansi inahitajika katika kuhakikisha kuwa wafugaji wanabadili ufugaji na kuwa na Mifugo Bora zaidi pamoja na mazao yenye thamani ambayo yanatokana na Mifugo.
“Tunahitaji Sana Sayansi ya Mifugo ambayo itatusaidia kupata nyama bora,maziwa bora na hata bidhaa nyingine zote ili basi idadi tuliyonayo ya Mifugo iendane na thamani ya Mifugo yetu na hivyo tutapata Mifugo Bora zaidi”alisema Profesa Ole Gabriel
Hata hivyo alisema kuwa uwepo wa maabara hizo mbili pamoja na vifaa vitawezesha wanafunzi hao ambao wanakwenda kusaidia wafugaji wa chini katika kuhamilisha na kuchanja Mifugo kubobea katika sekta hiyo na Mifugo kuwa Bora zaidi.
Pia alisema kuwa mpango wa wizara hiyo bado ni kuboresha kosafu na mbari za mifugo,ili kupata Mifugo bora na bidhaa bora zaidi na hatimaye kuchangia Uchumi kwa asilimia 15 tofauti na Sasa Ambapo sekta hiyo inachangia 7.64.
Nae Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vyuo vya Mifugo wa dkt.Pius Mwambene alisema kuwa vifaa hivyo vitawasaidia kuboresha mafunzo na kuhakikisha kuwa wanafunzi wanawasaidia wafugaji katika kubadili ufugaji wa mazoea.
Alisema kuwa ni azma ya Serikali kuhakikisha kuwa inaboresha miundombinu Mbali Mbali ili kuhakikisha kuwa sekta ya mifugo inachangia ipasavyo pato la taifa.
Nchi ya Poland imekuwa ikiisaidia Serikali katika sekta ya Mifugo katika kuhakikisha kuwa inaongeza thamani ya mifugo ili kuongeza tija katika sekta hiyo.