TBS YAWATAKA WAUZAJI WA MBAO KUUZA MBAO ZILIZOKIDHI VIWANGO VYA UBORA

 


WAUZAJI na wasambazaji wa mbao wametakiwa kuwasiliana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS,) ili waweze kuelekezwa ni viwango gani vinafaa kutumika kwenye bidhaa zipi za mbao na ni namna gani wanaweza kuzalisha ili waweze kuendana na matakwa ya viwango vya ubora.

Akizungumza na Mwandishi wetu Jijini Dar es Salaam, Afisa Viwango katika sekta ya Ujenzi na Majengo kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS,) Mhandisi Kakuru Chiganga amesema viwango vya ubora katika mbao vinakuwa vinaelezea muonekano wa nje ambao unaweza kukubarika na unakidhi ubora wa kimataifa.

"Mbao hizi tunapozitumia kuna muonekano ambao unakubarika maana kuna mbao zinatumika katika kutengeneza Furniture lakini kuna mbao zinatumika kwenye shughuli nyingine kwa mfano mirunda, kuezeka au kutengeneza fremu za madirisha na milango". Amesema Mhandisi Chiganga.

Aidha Mhandisi Chiganga amesema miongoni mwa matakwa mengine kwenye viwango vya ubora wa mbao ni uimara wa ubao wenyewe na bidhaa zinazotokana na mbao.

"Kuna matakwa ambayo yamekuwa yamewekwa kwaajili ya kuelezea uimara wa ubao na sehemu ambayo inaweza kutumika". Amesema Mhandisi Chiganga.

Sehemu nyingine ambayo imekuwa ikielezewa kwenye viwango vya ubora wa mbao ni uimara wa kupambana na unyevunyevu ambapo unaelezea kwamba ubao unatakiwa kuwa na unyevunyevu kiasi gani ili uweze kutumika sehemu na kudumu kwa muda mrefu

Post a Comment

Previous Post Next Post