KAZI YAANZA KYABAKARI KABLA YA SAA 24 ZILIZOTOLEWA NA KATIBU MKUU-MAJI

 

Mkurugenzi Msaidizi-Idara ya Usambazaji Maji , Wizara ya Maji Mhandisi Abbas Pyarali (kulia), akiongoza kikao baada ya kukabidhi eneo la ujenzi wa mradi maji wa Mugango-Kyabakari-Butiama kwa mkandarasi kampuni ya Unik.

Mkandarasi akipitishwa katika moja ya eneo ambalo atatakiwa kujenga tanki la kusambaza maji kwa wananchi. Katibu Mkuu, Wizara ya Maji alimtaka Mkandarasi kuanza kazi ndani ya saa 24 baada ya kusaini mkataba ili wananchi wapate huduma ya maji mapema.

Wawakilishi wa mkandarasi kampuni ya Unik, pamoja na wataalam wa Wizara ya Maji wakiangalia eneo ambalo litajengwa tanki jipya, na namna ya ulazaji bomba utakavyofanyika. Kazi ya utekelezaji wa mradi itafanyika sambasamba kwa kuhusisha maneo yote ya msingi, kujenga chanzo, mtambo wa kutibu maji, ulazaji wa mabomba na ujenzi wa matanki ya kuhifadhi maji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji ya Mugango – Kiabakari Mhandisi Cosmas Sanda (mwenye kofia) akionyesha eneo ambapo bomba la kusambaza maji kwa wananchi litapita. Mradi wa maji wa Mugango-Kyabakari-Butiama utatekelezwa kwa kipindi cha miezi 24. 

Post a Comment

Previous Post Next Post