Teknolojia ya kisasa ya tiba ya mionzi ya ELEKTA Harmony yaongeza matumaini kwa wagonjwa wa Saratani ORCI

Mashine ya tiba mionzi ya ELEKTA Harmony inayotoa huduma za matibabu ya saratani kwa kiwango cha kibingwa na ubingwa bobezi kwa kutumia teknolojia za kisasa za tiba mionzi. Serikali imeifunga mashine hiyo katika Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) ili kuboresha ubora, usahihi na ufanisi wa huduma za matibabu ya saratani nchini mradi uliogharimu shilingi bilioni 8.3.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) Dkt. Diwani Msemo akiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Computech Healthcare Solutions Hanif Popat na wafanyazi wa kampuni hiyo wakati wa ziara yao katika taasisi hiyo kwaajili ya kukagua mashine ya tiba mionzi ya ELEKTA Harmony inayotoa huduma za matibabu ya saratani kwa kiwango cha kibingwa na ubingwa bobezi kwa kutumia teknolojia za kisasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) Dkt. Diwani Msemo akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Computech Healthcare Solutions, Hanif Popat wakati wa ziara yake katika taasisi hiyo kwaajili ya kuangalia utendaji kazi wa mashine ya tiba mionzi ya ELEKTA Harmony. Mashine hiyo iliyofungwa na Kampuni ya Computech Healthcare Solutions inatoa huduma za matibabu ya saratani kwa kiwango cha kibingwa na ubingwa bobezi kwa kutumia teknolojia za kisasa.

Post a Comment

Previous Post Next Post