DKT. NCHEMBA AWASILISHA MAPENDEKEZO YA MFUMO NA UKOMO WA BAJETI KWA MWAKA 2025/2026

 

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwasilisha bungeni jijini Dodoma, Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2025/2026 kwenye Kamati ya Bunge zima, ambapo Serikali imependekeza kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 57.04 kwa mwaka 2025/26, sawa na ongezeko la asilimia 13.4 ikilinganishwa na Bajeti ya Mwaka wa Fedha, 2024/25 ya shilingi trilioni 50.29.
 Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa tatu kushoto mstari wa mbele) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, (wa tatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, na Tume ya Mipango, baada ya kuwasilisha Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2025/2026 kwenye Kamati ya Bunge zima, bungeni jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (wa pili kushoto mstari wa mbele), Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Mhe. Stanslaus Nyongo (wa pili kulia mstari wa mbele), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa kwanza kushoto mstari wa mbele) na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, baada ya kuwasilisha Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2025/2026 kwenye Kamati ya Bunge zima, bungeni jijini Dodoma, ambapo Serikali imependekeza kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 57.04 kwa mwaka 2025/26, sawa na ongezeko la asilimia 13.4 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2024/25 ya shilingi trilionin 50.29.
 Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Fedha, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, na Tume ya Mipango, wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani) wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2025/2026 kwenye Kamati ya Bunge zima, bungeni jijini Dodoma, ambapo Serikali imependekeza kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 57.04 kwa mwaka 2025/26, sawa na ongezeko la asilimia 13.4 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2024/25 ya shilingi trilionin 50.29.
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akiteta jambo na Manaibu Katibu watendaji wa Tume ya Mipango Dkt. Linda Ezekiel na Dkt. Lorah Madete, bungeni jijini Dodoma, baada ya hafla ya kuwasilisha Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2025/2026 kwenye Kamati ya Bunge zima, ambapo Serikali imependekeza kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 57.04 kwa mwaka 2025/26, sawa na ongezeko la asilimia 13.4 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2024/25 ya shilingi trilionin 50.29. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)
……..
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amewasilisha Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/26, kwenye Kamati ya Bunge zima, katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma, ambapo Serikali imependekeza kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 57.04 kwa mwaka 2025/26, sawa na ongezeko la asilimia 13.4 ikilinganishwa na Bajeti ya Mwaka wa Fedha, 2024/25 ya shilingi trilioni 50.29.
 
Hafla hiyo imeongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa na kuhudhuriwa pia na Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azan Zungu, na viongozi waandamizi wa Serikali.

Post a Comment

Previous Post Next Post