
Wakala wa Nishati Vijijini (REA), leo Machi 6, 2025 umeendelea kutoa elimu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia katika siku ya pili ya Kongamano na Maonesho ya Petroli ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAPCE’25) yanayofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa JNICC jijini Dar es Salaam.