Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Vipimo (WMA),Prof.Eliza Mwakasangula,akiwa na wajumbe wa bodi hiyo wakipata maelezo wakati wa ziara ya wajumbe wa bodi hiyo ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la WMA Makao Mkuu Dodoma,leo Februari 7,2025.
Na.Alex Sonna-DODOMA
BODI ya Ushauri ya Wakala wa Vipimo (WMA),imeridhishwa na kasi ya ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Makao Mkuu Dodoma ya wakala huo ambalo linatarajiwa kukabidhiwa Februari 10, mwaka huu.
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof.Eliza Mwakasangula,ameyabainisha hayo leo Februari 7,2025 jijini Dodoma mara baada ya ziara ya wajumbe wa bodi hiyo kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo.
Prof. Mwakasangula, amesema kuwa ziara hiyo ambayo imejumuisha wajumbe wa bodi ya ushauri ya WMA, lengo kuu lilikua ni kukagua ujenzi wa jengo hilo ambalo linagharimu kiasi cha Sh.bilioni 6.2.
“Ziara yetu hii leo pamoja na wajumbe hawa wa bodi ya ushauri ya WMA tumekuja kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi na kwa namna tulivyoona hapa tumeridhishwa na ujenzi na tunatarajia kulizindua wakati wowote”amesema Prof. Mwakasangula
Aidha, amemshukuru Waziri wa Viwanda na Biashara,Mhe.Dkt. Selemani Jafo na kamati yake kwa kusimamia kikamilifu ujenzi wa jengo hilo kukamilika kwa wakati.
“Lakini pia nimshukuru mtendaji mkuu wa WMA, kwa kusimamia ujenzi wa jengo hili bega kwa bega na kuhakikisha kwamba jengo hili linakamilika”amesema
Hata hivyo ameishukuru menejimenti ya WMA, kwa kuona umuhimu wa jengo hilo na kutenga bajeti kupitia fedha za ndani ambapo hadi sasa kiasi chote cha fedha Sh. Bilioni 6.2 kimeshalipwa na taasisi haidaiwi.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo Bw. Alban Kihulla, amesema kuwa lengo la ziara hiyo ni wajumbe wa bodi kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo ambalo litatumika kama makao makuu ya taasisi hiyo.
“Wajumbe wa bodi wameridhika na ujenzi wa jengo hili na hali hiyo inatupa matumaini ya kukabidhiwa jengo hili ndani ya siku hizi tatu ambapo hivi sasa kuna ukamilishaji wa shughuli ndogondogo ambazo ndani ya siku hizi tatu utakua umekamilika”amesema Kihulla
Hata hivyo, amesema jengo hilo limefikia zaidi ya asilimia 97 hivyo ni matumaini yake ndani ya siku hizo tatu watakua wamekabidhiwa.
Naye Mkandarasi wa Kampuni ya Mohamed Builders Bw.Burhan Hamza,ameipongeza WMA kwa kumpa kazi hiyo huku akiahidi kuwa mradi huo watakabidhi Februari 10 mwaka huu.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250207-WA00292-1024x683.jpg)
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Vipimo (WMA),Prof.Eliza Mwakasangula,akiwa na wajumbe wa bodi hiyo wakipata maelezo wakati wa ziara ya wajumbe wa bodi hiyo ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la WMA Makao Mkuu Dodoma,leo Februari 7,2025 jijini Dodoma.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250207-WA00301-1024x683.jpg)
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Vipimo (WMA),Prof.Eliza Mwakasangula,akiwa na wajumbe wa bodi hiyo wakipata maelezo wakati wa ziara ya wajumbe wa bodi hiyo ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la WMA Makao Mkuu Dodoma,leo Februari 7,2025 jijini Dodoma.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250207-WA00311-1024x683.jpg)
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Vipimo (WMA),Prof.Eliza Mwakasangula,akiwa na wajumbe wa bodi hiyo wakipata maelezo wakati wa ziara ya wajumbe wa bodi hiyo ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la WMA Makao Mkuu Dodoma,leo Februari 7,2025 jijini Dodoma.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250207-WA00341-1024x683.jpg)
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Vipimo (WMA),Prof.Eliza Mwakasangula (kushoto) akisikiliza maelezo wakati wa ziara ya wajumbe wa bodi hiyo ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la WMA Makao Mkuu Dodoma,leo Februari 7,2025 jijini Dodoma.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250207-WA00321-1024x683.jpg)
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Vipimo (WMA),Prof.Eliza Mwakasangula,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la WMA Makao Mkuu Dodoma,leo Februari 7,2025 jijini Dodoma.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250207-WA00351.jpg)
Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo Bw. Alban Kihulla,akizungumza ,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Vipimo (WMA) kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la WMA Makao Mkuu Dodoma,leo Februari 7,2025 jijini Dodoma.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250207-WA00361.jpg)
Mkandarasi wa Kampuni ya Mohamed Builders Bw.Burhan Hamza,akizungumza ,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Vipimo (WMA) kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la WMA Makao Mkuu Dodoma,leo Februari 7,2025 jijini Dodoma.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250207-WA00331-1024x683.jpg)
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Vipimo (WMA),Prof.Eliza Mwakasangula,(katikati)akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la WMA Makao Mkuu Dodoma,leo Februari 7,2025 jijini Dodoma.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250120-WA00641.jpg)
MUONEKANO wa Jengo la WMA Makao Mkuu Dodoma.