HAKUNA TRA BILA WAFANYABIASHARA - CG MWENDA

 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda amesema hakuna TRA bila kuwepo wafanyabaishara hivyo, TRA ina jukumu la kuhakikisha ustawi wa biashara nchini ili iendelee kuwepo na kukusanya kodi.

Ameyasema hayo wakati wa kikao na wafanyabiashara mkoani Ruvuma tarehe 13/02/2025 ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kuwatembelea wafanyabiashara, kuwasikiliza na kutatua kero za kikodi.

Bw. Mwenda amesema watakikisha hakuna biashara inayokufa na badala yake zinazaliwa nyingine ili kuongeza wigo wa ukusanyaji wa Kodi nchini.





Post a Comment

Previous Post Next Post