Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda akiwa ziarani wilayani Igunga mkoani Tabora February 06 mwaka huu amepita mlango kwa mlango kwa Wafanyabiashara kwa lengo la kuwashukuru, kuwasikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili.
Kamishna Mkuu Mwenda akiambatana na Uongozi wa TRA alifika katika baadhi ya maduka na kutoa shukurani pamoja na elimu ya kodi ambapo aliwahakikishia Wafanyabiashara aliokutana nao kuwa, TRA ipo mahsusi kulinda biashara zao.
Kamishna Mkuu Mwenda amesema bila Wafanyabiashara hakuna Kodi hivyo kipaumbele chao kikubwa ni kuboresha biashara halafu ndiyo masuala ya kodi yanafuata.
Katika hatua nyingine Kamishna Mkuu Mwenda amewapongeza Walipakodi wa Igunga kwa kuendelea kuwa na Imani na TRA na kulipa Kodi kwa hiari maana wamekuwa wakichangia Maendeleo ya Taifa katika kila sekta.
Kamishna Mkuu Mwenda amekuwa na utaratibu wa kupita kwa Walipakodi na kuzungumza nao tangu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo jambo ambalo limeongeza zaidi imani ya Walipakodi kwa TRA.