KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAJI

 



Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira inayoongozwa na Mwenyekiti Mhe. Jackson Kiswaga (Mb) imeipa Kongole Wizara ya Maji baada ya kuridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maji nchini.

Pongezi hizo zimetolewa leo Januari 22, 2025 wakati wa kuhitimisha vikao vya kamati hiyo jijini Dodoma.

Kamati imetoa Pongezi hizo baada ya kupokea taarifa iliyowasilishwa na Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) kuhusu hali ya upatikanaji wa Maji nchini hadi Disemba 2024.

Mwenyekiti kiswaga amesema kazi kubwa imefanyika katika kukamilisha miradi na kuwafikishia wananchi huduma ya majisafi na salama lengo likiwa kufikia azma ya serikali ambayo ni kufikisha huduma ya majisafi na salama kwa 95% mjini na 85 vijijini.

Mhe. Aweso amesema hadi kufikia
Disemba 2024 Hali ya
Upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama Vijijini ilikuwa imefika 83%, wakati mijini huduma imefikia 91.6%.

Aidha kamati imempongeza Waziri Aweso kwa kuendelea kuiongeza wizara kwa ufanisi mkubwa.

Mwisho ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongizwa na Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji nchini kote.



Post a Comment

Previous Post Next Post