“MA DGO UNGENI MKONO JUHUDI ZA RAIS SAMIA”. DKT ABBASI

 

……,…………..

Na Sixmund Begashe -Dodoma

Maafisa Wanyamapori wa Wilaya nchini (DGOs) wametakiwa kuunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uhifadhi wa Maliasili kwa maslahi mapana ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi alipokuwa akifunga kikao kazi cha siku mbili cha Maafisa hao na Wizara hiyo Jijini Dodoma.

Dkt. Abbasi amesema, kupitia jitihada za Mhe. Rais Samia katika uhifadhi, kwa mara ya kwanza ameridhia asilimia tatu kutoka kwenye mapato ya TAWA, TANAPA na Ngorongoro ziingie kwenye mfuko wa Wanyamapori, ambao kimsingi unawakuza Maafisa Wanyamapori wa Wilaya nchini.

“Tumekuwa na changamoto kubwa ya kujitangaza Duniani ili Dunia ijue na ije Tanzania lakini Mhe. Rais pamoja na fedha za maendeleo amefanya uwamuzi mkubwa na wakimkakati wa kudhiria fedha kiasi cha asilimia 6 ya Mapato yote ya TANAPA, TAWA na Ngorongoro yabaki kwenye mfuko wa Maendeleo ya Sekta ya Utalii” aliongeza Dkt. Abbasi

Aidha Dkt. Abbasi amewataka Maafisa hao kuhakikisha wanabuni kazi za kusaidia kutatua changamoto zilizopo kwenye uhifadhi zitakazo wezeshwa na mfuko wa Wanyamapori kwa maslahi mapana ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Dkt. Abbasi licha ya kuwapongeza Maafisa hao kwa kazi nzuri wanazofanya, amewakumbusha wajibu wao hususani uadilifu pindi wanapotekekeza majukumu yao, kujituma, na kushirikiana vyema na Taasisi za Wizara katika maneno yao

Naye Katibu wa Maafisa Wanyamapori hao Bw. Nicodemus Mombia, ameushukuru uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kikao hicho cha kihistoria kwani kimeweza kuwapatia uwelewa mpana juu ya majukumu yao na kuongeza mshikamano baina yao na Wizara hali itakayo ongeza ufanisi kwenye utekelezaji wa majukumu yao.

Kikao hicho kilichofunguliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, kimehudhuriwa pia na viongozi waandamizi wa Wizara hiyo, na kuwa kitakuwa kikifanyika kila Mwaka.

Post a Comment

Previous Post Next Post