Wakulima watakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya mbolea

 Na Mwandishi Wetu,

Wakulima wametakiwa kutumia teknolojia bora za kilimo kuzalisha kwa tija ikiwemo matumizi sahihi ya mbolea.

Hayo yamezungumzwa na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania Dkt. Anthony Diallo alipokamilisha mbio za mbolea mjini Babati katika kilele cha siku ya mbolea duniani.

Dkt. Diallo amesema zipo teknolojia mbalimbali za kilimo zinazosaidia tija ya mavuno ikiwemo matumizi ya mimea kufukuza visumbufu vya mazao.

Aidha ameongeza kuwa mmea unahitaji kupata chakula sahihi ambacho kinatokana na matumizi sahihi ya mbolea na kuwataka wakulima kutumia kilele cha maadhimisho ya siku ya mbolea kujifunza mbinu za kilimo bora.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA Joel Laurent amesema kuwa TFRA imeleta mbio za mbolea kuhamasisha matumizi sahihi ya mbolea kupitia michezo.

Ameongeza kuwa kilimo kinahusisha afya hivyo pamoja na mambo mengine wakulima waliopata fursa kushiriki mbio za mbolea wamenufaika kwa kujenga afya pamoja na kupata elimu ya matumizi sahihi ya mbolea.

Oktoba 13 kila mwaka ni siku ya Mbolea Duniani ambayo kiraifa inafanyika mjini Babati ikitanguliwa na Mbolea day fun run iliyowakutanisha pamoja wakulima na wadau wengine wa tasnia ya mbolea kujenga afya ya mwili na kubadilishana uzoefu.



Post a Comment

Previous Post Next Post