BALOZI KASIKE AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA TANTRADE

 

Mkutano huo ulifanyika kwenye Ofisi za TANTRADE zilizopo kwenye Viwanja vya Sabasaba, Dar es Salaam ambapo Viongozi hao wawili walikubaliana kushirikiana katika kutafuta Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka nchini Msumbiji kwa ajili ya kuja kuwekeza na kufanya Biashara nchini Tanzania. Wakati wa mkutano huo, TANTRADE iliahidi kushiriki katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Jijini Maputo (FACIM) yatakayofanyika Msumbiji mwezi Agosti, 2024 sambamba na Wadau wengine ili kutangaza fursa mbalimbali za kibiashara na Uwekezaji zilizopo Tanzania.

Kwa upande wake, Mhe. Balozi Kasike aliahidi kutoa kila aina ya ushirikiano kwa TANTRADE ili kuwafikia Wafanyabiashara na wadau wengine muhimu waliopo Msumbiji ili kuja kuwekeza nchini Tanzania.

Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania – Maputo

Post a Comment

Previous Post Next Post